Papa jana ameonesha hakika ni mtu wa watu baada ya kuachana na gari binafsi la Vatican na kupanda basi badala yake.
Inaaminika picha hiyo ilipigwa wakati Papa akisafiri kutoka hoteli ya Vatican kwenda kuendesha ibada katika Kanisa Dogo la Sistine.
Katika siku chache tangu alipochaguliwa, Papa Francis I ameonesha mambo mengi ya kujishusha kwake na kuendeleza asili yake.
Baada ya kuwa amekaa katika makazi ya mapadri kabla ya upigaji kura katika mkutano wa faragha, Papa Francis I alisisitiza kurejea na kulipa fadhila pamoja na kutaka kuwashukuru wafanyakazi kwa ukarimu wao.
Wengi wamesema kwamba Baba Mtakatifu huyo mpya ni tofauti kabisa na aliyemtangulia Benedict XVI kwamba tayari anaikabili kazi hiyo katika utamaduni wa chini na tabia nyingi tofauti.
Katika hotuba yake ya kwanza, alitoa taarifa muhimu na hotuba ya kuelimisha kwa Kardinali, si kwa Kilatini, lakini kwa Kitaliano.
Na mara alipojitokeza kwenye kibaraza cha Kanisa la Mt. Petro baada ya kuwa amechaguliwa kuwa mkuu mpya wa Kanisa Katoliki, aliusalimia umati kwa kusema tu: "Kaka na dada, habari za jioni."
Wakati akiwa kama Askofu Mkuu mjini Beunos Aires mara kwa mara alikuwa akipanda basi wakati akisafiri kwenda kwenye baadhi ya maeneo maskini kabisa kuendesha ibada.
Pia alichagua kuishi kwenye nyumba ndogo, akiachana na makazi mengi ya kifahari.
Wakati huohuo Vatican imeshambulia vikali kile ilichoita kampeni 'chafu' kumuaibisha Papa Francis dhidi ya madai ya kuufumbia macho utawala wa kidikteta nchini Argentina.
"Hakujawahi kuwapo shutuma nzito na za uhakika dhidi yake," alisema msemaji wa Vatican Federico Lombardi, akiongeza kuwa kamwe hajawahi kushitakiwa.
Ukanushwaji huo dhidi ya 'Vita Chafu' ya Argentina umekuja baada ya Papa Francis kutumia muda wa asubuhi kuongea na makardinali wake katika Bwalo la Clementine la Jumba hilo la Kitume.
Papa huyo mwenye miaka 76 alijikwaa wakati akishusha ngazi kutoka altareni kuwasalimu makardinali hao - ilionekana kama kiatu chake cha mguu wa kushoto kilijitega kwenye joho lake jeupe lililokuwa likining'inia.
Haraka alimudu kuziweka sawa hatua zake, lakini si kabla ya safari yake hiyo kunaswa kwa ajili ya dunia kushuhudia.