Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

AFARIKI BAADA YA KUNYWA GONGO SIKU MBILI MFULULIZO KATAVI...

$
0
0
Kamanda Dhahiri Kidavashari.
Mkazi  wa Mtaa wa Mpanda Hoteli  mjini Mpanda,  Aloyce Sali (32) amefariki dunia baada ya kunywa pombe  haramu  ya  gongo kupita kiasi  kwa siku  mbili mfululizo  bila kula chakula chochote.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari  alisema kifo cha mtu huyo kilitokea juzi   saa 4:30 nyumbani kwake, mtaa huo wa Mpanda Hoteli  ambako alikuwa amepanga chumba.
Kwa mujibu wa kamanda, kabla ya  tukio, Sali aliondoka  nyumbani kwake saa 7 mchana na kwenda kilabu cha kuuza pombe za kienyeji inayomilikiwa na mtu anayetambulika kwa jina moja la Mwandosya, Mtaa wa Mpanda Hoteli.
“Alianza kunywa pombe hiyo ya gongo kwa siku mbili  mfululizo  bila  kula  chakula  chochote,” alisema kamanda.
Inadaiwa alirudi nyumbani usiku na kulala. Wapangaji wenzake  walipoona imefikia  saa 6 mchana,  walipata wasiwasi ndipo  walipovunja  mlango  wa  chumba  chake  na  kubaini amefariki.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles