![]() |
Paulo Henrique Machado akiwa kitandani hospitalini hapo. |
Paulo Henrique Machado ametumia maisha yake yote akiwa hospitalini.
Mtu huyo mwenye miaka 45 raia wa Brazil, ambaye mama yake alifariki siku mbili baada ya kumzaa, alishambuliwa na maradhi kupooza kitoto yaliyosababishwa na polio, yakimwacha akiwa hana uwezo wa kujihudumia mwenyewe.
Anahitaji msaada wa kila kitu huku akipumua kwa kutumia chombo maalumu, hawezi kutembea bila kusaidiwa.
Lakini licha ha hali yake ya kudhoofika, Paulo amejifunza uhuishaji kwa kutumia kompyuta na anatengeneza filamu kuhusu maisha yake, kutokana na stori iliyoandaliwa na rafiki yake mkubwa, msiri wake na mwenzake wodini, Eliana Zagui, ambaye pia aliathirika na polio alipokuwa mtoto na ameishi hospitalini hapo tangu wakati huo.
"Baadhi ya watu hudhani sisi ni kama mume na mke, lakini sisi zaidi ni kaka na dada," alisema Paulo. "Kila siku, ninapoamka nafahamu kwamba nguvu yangu iko pale -Eliana. Na inafidia. Ninamwamini na yeye ananiamini."
Wawili hao walikuwa miongoni mwa watoto 11 waliolazwa hospitalini hapo kwa maradhi ya polio - ugonjwa wa kuambukiza ambao huathiri watoto wenye umri chini ya miaka mitano - katika miaka ya 1970.
Akilazimishwa kuishi katika kile kilichoitwa 'torpedo' - haraka mwili ukipandikizwa mapafu ya chuma - katika miaka yake ya mwanzoni, alitengeneza ulimwengu wake mwenyewe ndani ya hospitali hiyo pamoja na marafiki zake.
Kumbukumbu zake za awali ni za 'kukagua' vibaraza vya hospitali akiwa kwenye kiti cha magurudumu, kuingia kwenye vyumba vya watoto wengine na kutumia hisia kutengeneza 'ulimwengu' wake mwenyewe.
Lakini, huku wakiwa wamepishana takribani miaka 10 katika maisha yao, Paulo na Eliana wanajishuhudia wote wakifa, mmoja baada ya mwingine.
Madaktari wameshindwa kabisa kufahamu kwanini Paulo na Eliana wameishi muda mrefu zaidi ya wengine, lakini wanasema uzoefu, wakati wa huzuni kubwa, umewafanya wawe karibu pamoja.
"Ilikuwa vigumu," anasema Paulo. "Hasara yoyote ilikuwa kama kukatwa viungo, unafahamu, kimwili ... kama kuharibu. Sasa, tumebaki wawili tu kati yetu - mimi na Eliana."
Hatari ya maambukizo ni kubwa kwa Paulo na Eliana, hivyo wamekuwa wakisafiri mara chache nje ya hospitali hiyo.
Lakini maendeleo ya teknolojia yanawaruhusu kuongeza uhuru wa kuona sehemu za dunia ambazo watu wa hali ya chini huziona kwa nadra.
Hatahivyo walifanya safari kadhaa nje; kubwa kabisa ya kukumbukwa ilikuwa walipoenda ufukweni katika miaka ya 1990.
"Kuna baadhi ya safari ambazo hazitasahaulika, kama kwenda ufukweni kwa mara ya kwanza wakati nilipokuwa na miaka 32," anasema.
"Nilifungua mlango wa gari na kuona bahari na kushangaa 'Wow! Hiki nini?'"
Eliana, ambaye husema alijenga picha ya bahari kutokana na filamu, picha na postikadi, aliongeza: "Walituchukua kwenye gari, Paulo alikuwa kwenye kiti cha magurudumu na wakasukuma kitanda changu ndani ya mchanga.
"Unafurahia matukio haya madogo, ambao watu wengi huyapata kwa nadra. Hawaachi kushangaa kama tulivyofanya sisi."
Sababu walikuwa wameishi katika hospitali hiyo kwa muda mrefu mno, wanaruhusiwa kupamba chumba chao kwa namna yoyote wanayochagua. Wakati wakisema mara kadhaa wamekuwa wakiingia kwenye malumbano ya kirafiki, wamekubaliana kugawa chumba hicho katikati.