Habari zilizopatikana muda mfupi uliopita zinasema, Robert Mugabe ameshinda theluthi mbili ya viti vyote vya ubunge katika uchaguzi uliofanyika wiki hii nchini Zimbabwe - ambao makundi mawili makubwa ya waangalizi kutoka Afrika yamethibitisha 'huru na wa amani'.
Kura hizo zilipigwa kati ya mkanganyiko mkubwa kuhusu madai ya kutapakaa udanganyifu mkubwa na wizi wa kura.
Ilipelekea kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai kuita uchaguzi huo 'kichekesho kikubwa' na ‘null and void’.
Lakini Umoja wa Afrika ulitupilia mbali madai hayo ya udanganyifu, wakati mwangalizi mwingine aliasa vyama vyote 'kukubali mazingira magumu'.
Rais huyo mwenye miaka 89, ambaye anaongoza kwa kipindi chake cha saba, amekuwa mtawala wa Zimbabwe tangu ilipopata uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka 1980.
Olusegun Obasanjo, mkuu wa ujumbe wa Afrika, alikiri kulikuwa na 'matukio ambayo yangeweza kuepukika' lakini alisema haya hayawezi kuharamisha matokeo ya jumla ya kura hizo.