![]() |
Waziri Mkuu Mizengo Pinda. |
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, amesema haoni mantiki yoyote au uhalali wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), kumshitaki Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Alisema hayo juzi wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari, baada ya kufungwa kwa mkutano wa siku tatu wa mawakili wa Serikali wafawidhi, wakuu wa upelelezi wa mikoa na vikosi vingine vya Polisi.
Alisema kauli aliyotoa Pinda bungeni, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu kuhusu Polisi kutumia nguvu kwa wananchi, ililenga wanaokaidi kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria na si kupiga na kuua kama ilivyotafsiriwa na wengi.
“Sijapata taarifa kwa maandishi juu ya azma ya kumshitaki Waziri Mkuu, lakini Pinda hajavunja sheria kwa kauli yake aliyotoa,” alisema.
Alisema kwa jinsi alivyosikia maelezo ya Waziri Mkuu bungeni, kama LHRC wanamshitaki kwa jinai Waziri Mkuu, haoni uhalali wa mashitaka hayo.
Alisema Waziri Mkuu alieleza hatua zinazochukuliwa dhidi ya mvunja sheria, na kufafanua kuwa Mtanzania yeyote ana haki kwa mujibu wa sheria, lakini pia ana wajibu, ndiyo maana vipo vyombo na kila chombo kimepewa mamlaka na wajibu wa kutekeleza.
Alifafanua, kwamba kilichoongelewa ni dhana ya mkusanyiko ambayo ni haki kwa mujibu wa Katiba, ikiwemo uhuru wa kukutana, kutoa mawazo na kufanya mawasiliano.
Hata hivyo, alikumbusha kuwa Sheria ya Jeshi la Polisi, inasema ili mkusanyiko ufanyike, lazima taarifa itolewe kwa kiongozi wa Polisi wa eneo husika.
Sheria hiyo inasema, kama mkusanyiko una nia ya kutenda kosa na ikafanyika hivyo, kuna chombo kilichopewa dhamana ya kuhakikisha mkusanyiko haramu unatawanyika na sheria hiyo inaruhusu Polisi kutawanya mkusanyiko haramu.
“Unatarajia nini kama kuna watu wanafanya fujo na polisi wana mamlaka ya kuwakamata waliofanya fujo?” Alihoji Feleshi na kuongeza kuwa dhana ya matumizi ya nguvu ni ya kisheria pia.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, akizungumza kwa simu na mwandishi, alisema utaratibu wa Polisi kulazimika kutumia nguvu upo.
Aliutaja utaratibu huo kwamba unatumika hasa katika mikusanyiko isiyotakiwa, ambapo Polisi hulazimika kutoa tangazo la angalizo mara kadhaa kutaka watu watawanyike.
“Tangazo linapotolewa, Polisi kwa kutumia kipaza sauti husema, tawanyikeni, tawanyikeni na kusisitiza hivyo mara kadhaa, hapo wanaopaswa kutawanyika wakikaidi, nguvu hutumika ingawa inaweza isiwe ya kupiga risasi, pengine virungu, yote hiyo si kupiga?
“Risasi ni kitu cha mwisho, labda uwe unashambuliwa wewe (polisi), hata ikiwa hivyo, ukipiga risasi kuna maeneo ya kupiga, si kichwani, polisi wana mafunzo ya kupiga maeneo ya miguuni, hivyo kutumia nguvu kwa polisi kupo,” alisema Jaji Werema.
Feleshi alisema sheria inayoelezea dhana hiyo ni pamoja na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, ambayo imeeleza wakati upi mtu anakamatwa baada ya kupatikana kwa hati ya kukamatwa, na wakati upi anakamatwa bila kuwepo hati hiyo.
Alisema kama mtu hana shari, hakuna mahitaji hata ya kumgusa, anaambiwa anahitajika kituoni na anakwenda, lakini kama anakataa, sheria inaruhusu matumizi ya nguvu.
Alihoji Waziri Mkuu kusema watu watakaokaidi kufuata utaratibu hatua za kisheria zichukuliwe, kosa ni lipi? Aliongeza kuwa neno kupiga, lazima lipewe maana na haliwezi kutumika kwa mtu ambaye hajavunja sheria.
“Neno kupigwa nilivyoelewa mimi, ni sawa na mtu ambaye anaamua kumshambulia askari, ulitarajia askari afanye nini?
“Sidhani kama kauli ya Waziri Mkuu inatakiwa ichukuliwe kama
alikuwa anahalalisha piga ua, hapana, mimi sikuelewa hivyo,” alisema Feleshi.
Wakati vigogo hao wa sheria serikalini wakiweka wazi usahihi wa Pinda, LHRC, imefungua kesi mahakamani kupinga kauli ya Pinda kuhusu Jeshi la Polisi kupiga raia wanaokaidi amri halali ya Jeshi hilo.
Kesi hiyo ilifunguliwa jana asubuhi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kusajiliwa kwa namba 24 ya mwaka 2013, baada ya shinikizo la wanaharakati hao kutaka Pinda afute kauli hiyo, kushindwa.
Katika kesi hiyo, kituo hicho kimeungwa mkono na taasisi nyingine zisizo za Serikali, kuwashitaki Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, kituo hicho kinadai Mei 20, Pinda akiwa bungeni Waziri Mkuu, kinyume na Katiba ya Nchi alitoa kauli ya kuruhusu askari Polisi kupiga raia ambao hawatatii amri yao kunapokuwa na vurugu.
“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi, watakupiga tu na mimi nasema muwapige tu kwa sababu hakuna namna nyingine, eeh maana tumechoka sasa,” sehemu ya hati hiyo ilinukuu kauli ya Pinda.
Katika hati hiyo, wanadai kwa mujibu wa utekelezaji wa Sheria za Jinai, kauli inayotolewa na kiongozi-Waziri Mkuu, inaonekana kama amri inayopaswa kutekelezwa na vyombo vya Dola kama Polisi.
Wanadai kwa uelewa wao, polisi watadhani ni amri halali iliyotolewa na kiongozi wao na kusababisha waendelee kutesa na kupiga wananchi wasio na hatia, kinyume na haki iliyowekwa kwenye sheria.
Kituo hicho kinadai kauli ya Pinda inahatarisha haki ya kuishi, inadhalilisha utu wa mtu, inaunga mkono matumizi mabaya ya utekelezaji wa kisheria, inasababisha ukiukwaji wa haki ya kusikilizwa na kumdhalilisha mtu ambaye ameshikiliwa na vyombo vya Dola.
Wanadai alivunja ibara ya 100 ya Katiba, inayompa kinga mbunge anapotoa jambo lolote bungeni, kwa kuwa yeye hakuzungumza bungeni kama mbunge, bali alikuwa anatoa msimamo wa Serikali.
Akizungumza baada ya kusajili kesi hiyo, Mkurugenzi wa Kituo hicho, Hellen Kijo-Bisimba, alidai kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Tanzania Bara (TLS), wananchi na taasisi mbalimbali, wameamua kumshitaki Pinda kwa kuwa hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria.
“Mtu yeyote anayevunja Katiba, anatakiwa kushitakiwa na sehemu ya kumshughulikia ni mahakamani,” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Raia inayofuatilia mwenendo wa Bunge, Marcosy Albanie, alisema tamko alilotoa Pinda linavunja Katiba.