Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

MWAROBAINI WA KUPAMBANA NA UJAMBAZI WAPATIKANA...

$
0
0
Baadhi ya silaha zilizokamatwa na polisi kwenye moja ya matukio ya ujambazi hapa nchini.
Jeshi la Polisi nchini katika kupambana na uhalifu limekuja na mbinu mpya ya kutambua wahalifu kwa kutumia gari maalumu ambalo lina uwezo wa kuchukua taarifa, alama za vidole na picha katika matukio ya uhalifu na kuzihariri.

Taarifa hizo na alama za vidole polisi ikishachukua inashirikiana na taasisi nyingine kama Ofisi ya Mkemia Mkuu kuweza kumbaini mhalifu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema alikabidhiwa gari hilo lenye utambuzi huo jana jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Uturuki, Zeki Gatalika.
Mwema alisema gari hilo ni msaada mkubwa kwa jeshi hilo katika kuwabaini wahalifu na kuthibitisha matukio hayo bila kuacha shaka yoyote.
Alisema gari hilo lina vitu vya kuchukua alama za vidole kibaolojia ili kuweza kutambua vinasaba (DNA) vya mtuhumiwa ambavyo vitatoa ushahidi hata kama hakukuwa na mtu kwenye eneo la tukio aliyeshuhudia wakati uhalifu ukitendeka.
"Gari hili ni msaada mkubwa kwetu na hasa katika kipindi hiki ambacho  jeshi litakuwa la kisasa, kupitia gari hili kuna uwezekano hata kama mhalifu alitema mate katika tukio basi mate yake yatatusaidia kumjua ni nani tukishirikiana na ofisi ya mkemia wa Serikali," alisema Mwema.
Alisema Serikali ya Uturuki na ya Tanzania ziliingia mikataba mbalimbali ya ushirikiano ambapo katika hilo Jeshi la Polisi likachukua fursa ya kusaidiana katika kutokomeza uhalifu ambao ni kikwazo katika maendeleo.
Alisema kesi nyingi zinakwama mahakamani kutokana na kukosa ushahidi wa kutosha wa bila kuacha shaka yoyote kumtia mtuhumiwa hatiani hivyo kwa kupitia gari hilo maalumu na utaalamu wanaoendelea kujifunza Uturuki ili kukabiliana na matukio kwa weledi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mwamini Malemi aliishukuru Uturuki kwa msaada huo  na kusema anatarajia kutakuwa na mabadiliko makubwa katika idara ya uchunguzi.
Alisema maofisa wa Jeshi hapa nchini watakwenda Uturuki kupata mafunzo ya uchunguzi wa uhalifu na pia maofisa wa Uturuki watakuja hapa nchini kuona kile kinachofanyika na kutoa mbinu zinazofaa zaidi kukabiliana na uhalifu.
"Tumepewa gari ambalo litakuwa linachukua taarifa ikiwa ni pamoja na picha katika matukio ya uhalifu na kuzihariri hivyo mtu sio rahisi kukataa au kukwepa kwamba hakuwa yeye," alisema.
Katika siku za hivi karibuni uhalifu umerejea kwa kasi  nchini kwa kuripotiwa matukio kadhaa ya majambazi kutumia silaha na kuuwa na kujeruhi wananchi. Kwa Dar es Salaam pia polisi wamebaini kuwepo kiwanda cha kutengeneza silaha.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

Trending Articles