Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4630

BILIONEA WA MADUKA YA HOME SHOPPING CENTER AMWAGIWA TINDIKALI USONI...

$
0
0
Moja ya maduka ya Home Shopping Center lililoko katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Mfanyabiashara maarufu nchini anayemiliki mtandao wa maduka ya vifaa vya nyumbani ya Home Shopping Center (HSC), Said Mohamed Saad, amejeruhiwa usoni na kitu kinachodhaniwa kuwa ni tindikali.

Kutokana na shambulio hilo, inaelezwa macho yote ya mfanyabiashara huyo yamedhurika, moja likiwa zaidi.
Tukio hilo limethibitishwa na Jeshi la Polisi, kupitia Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kinondoni, Yussuf Mrefu.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mrefu alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2 usiku karibu na Kambi ya Polisi Oysterbay.
Alisema Mohammed alikumbwa na mkasa huo wakati akizungumza na wafanyakazi katika duka lake hilo lililopo Jengo la Msasani City Mall, Msasani jijini Dar es Salaam.
"Siwezi kusema moja kwa moja kama ni tindikali au la! Kwa sababu kuna wataalamu ambao wanaweza kujua kama ni tindikali au ni maji ya aina gani ambayo yanaweza kumdhuru binadamu," alisema Kamanda Mrefu.
Aliongeza kuwa, baada ya tukio hilo, bilionea huyo alilazwa katika Hospitali ya Trauma (AMI), kwa matibabu zaidi, ambapo Kamanda Mrefu alisema alijeruhiwa usoni.
Hata hivyo alisema hali yake si mbaya kwani baada ya tukio hilo aliweza kufika katika kituo cha Polisi kilichopo jirani na kutoa taarifa. Alisema bado wanaendelea kumtafuta mhusika kutokana na Mohamed kutambua taswira ya mtu huyo.
"Alisema kwamba mtu huyo ambaye ni mwembamba na mrefu alifika dukani kwake na kutoa kichupa kidogo mfukoni na kummwagia usoni, kisha kukimbia.
"Kwa hiyo upelelezi unaendelea kuhakikisha tunamkamata mtuhumiwa sahihi. Kazi ya kumsaka mtuhumiwa, tena kwa kasi kubwa inaendelea," aliongeza Kamanda Mrefu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4630

Trending Articles