Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

KARDINALI WA ARGENTINA ACHAGULIWA KUWA PAPA MPYA...

Image may be NSFW.
Clik here to view.
Kardinali Jorge Mario Bergoglio "Papa Francis I".
Habari zilizopatikana muda mfupi uliopita kutoka Vatican zinasema Kardinali Jorge Mario Bergoglio, mwenye umri wa miaka 76, kutoka Argentina amechaguliwa kuwa Papa Mpya wa Kanisa Katoliki duniani.
Maelfu ya Wakatoliki walikusanyika chini ya miamvuli nje ya Kanisa Kuu la Mt. Petro, wakisubiri kwa shauku kujitokeza kwa Baba Mtakatifu wa 266 wa kanisa hilo na kutoa ahadi ya utii kutokea kwenye kibaraza.
Papa huyo mpya atamrithi Benedict XVI, ambaye kujiuzulu kwake ghafla mwezi uliopita kuliwafanya makardinali 115 wa Kanisa Katoliki kuanzisha mkutano wa faragha, kuchagua kiongozi mpya wa Wakatoliki takribani bilioni 2 duniani kote.
Bergoglio atakuwa Papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini, eneo la dunia lenye Wakatoliki milioni 480. Alishinda theluthi mbili muhimu za kura baada ya siku mbili tu za mkutano huo wa faragha. Wagombea wengine kadhaa walihesabiwa kama washindi wa pili, akiwamo Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson, ambaye angeweza kuwa Papa wa kwanza Mwafrika katika zama hizi za sasa.
Kiongozi huyo mpya wa kanisa anachukua taasisi hiyo ambayo wengi wanasema iko kwenye matatizo makubwa, kutoka madai ya kumomonyoka kwa maadili kufuatia vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, ingawa baadaye suala hilo lilisambaa hadharani mbele ya kipindi cha upapa cha Benedict.
Baadhi ya vyanzo vya habari vimesema Kanisa Katoliki nchini Marekani limelipa kiasi cha Dola za Marekani bilioni 3 kumaliza madai ya udhalilishaji huo wa kijinsia, japo wengine wanakadiria pungufu ya bilioni.
Benedict XVI alisema katika ziara yake nchini Marekani mwaka 1998 kwamba alikuwa akifadhaishwa mno na skendo ya udhalilishaji kijinsia, na kuhakikisha kwamba kanisa hilo halitaruhusu wanaojihusisha na ngono kwa watoto kuwa mapadri.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

Trending Articles