![]() |
Baadhi ya abiria wa treni wakijipatia mahitaji yao njiani. |
Zaidi ya abiria 1,200 waliokuwa wakisafiri kwa njia ya treni kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam, wamekwama mjini hapa kutokana na mafuriko kung’oa tuta la reli eneo la Godegode, katika Wilaya ya Mpwapwa.
Mkasa wa abiria hao kukwama Dodoma, umeelezwa kuwa si wa kwanza kwani tangu waondoke Kigoma Jumapili iliyopita, wamekwama mara kadhaa.
Baadhi ya abiria wakizungumza na waandishi wa habari, walisema kuwa walitoka Kigoma Jumapili na kutarajia kufika Dar es Salaam Jumanne lakini treni hiyo iliharibika na kulazimika kulala njiani eneo la Isinga huko Tabora.
Mmoja wa abiria hao, Issa Kapolwa, alisema tangu waondoke Kigoma wamekuwa wakikwama njiani na sasa wamekwama mjini Dodoma na hawajui hatma yao.
Alisema kuwa wametangaziwa kuwa katika Stesheni ya Godegode, reli imejaa maji na mpaka sasa hakuna ushahidi wataondoka lini na mchana wa jana walitangaziwa wajipange kwenye madirisha ili wapatiwe fedha za kujikimu.
Abiria mwingine Hassan Ayub, alisema kuwa sasa ni siku ya tatu wako njiani na juzi walilala porini Tabora na walipouliza, waliambiwa injini ni mbovu sasa wamefika Dodoma wamekwama tena. Alisema bado usafiri wa reli hauridhishi na kuiomba Serikali kuboresha zaidi usafiri huo ambao unatumiwa na watu wengi.
Hata hivyo msimamizi wa Kituo cha Reli cha Dodoma, Celsus Roman, alisema treni hiyo iliyoingia Dodoma jana saa tano na nusu asubuhi , haikuruhusiwa kuendelea na safari kutokana na maji kujaa kwenye stesheni za Mgandu, Msigalu, Gulwe na Godegode.
Alisema pamoja na maeneo hayo kujaa maji, tuta la reli limesombwa na sasa mafundi wanashughulikia tatizo hilo.
Aidha alisema Kampuni ya Reli (TRL) makao makuu, imeagiza kila abiria apewe fedha za kujikimu Sh 2,500 na kuwa treni hiyo inatarajia kuendelea na safari yake leo.
Pamoja na kupatiwa fedha hizo za kujikimu, baadhi ya abiria hasa wenye watoto wamesema hazitoshi kwani wanalazimika kutafuta maji ya kufulia nguo za watoto ambazo wanazianika kwenye majani kando ya kituo hicho cha reli .
Wengine walilalamika kukosekana kwa huduma ya choo ambapo, wanalazimika kutumia vyoo vya kulipia, ambapo wamekuwa wakilipa Sh 200 huku wengine wakisema hawajaoga tangu Jumapili walipotoka Kigoma.