Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

WAZEE WALIOTESWA VITA VYA MAU-MAU KULIPWA FIDIA DOLA MILIONI 14...

$
0
0
Baadhi ya wazee hao wakiwa nje ya mahakama.
Uingereza imekubali kulipa fidia ya mamilioni ya Dola za Kimarekani kwa maelfu ya Wakenya walioteswa na majeshi ya kikoloni wakati wa mapinduzi ya mwisho wa Himaya ya Uingereza, mwanasheria na shuhuda wa kimataifa alisema jana.

Makubaliano yalianza baada ya mahakama ya London kutoa uamuzi Oktoba kwamba wazee watatu raia wa Kenya, ambao waliathirika na ubakaji na vipigo wakati wakiwa kizuizini wakati wa mashambulizi ya majeshi ya Uingereza na vikosi vyao vya Kenya katika miaka ya 1950, wanaweza kuishitaki Uingereza.
Mateso hayo yalifanyika wakati wa 'Dharura' maarufu nchini Kenya ya miaka ya 1950-60, pale wapiganaji kutoka kwa askari hao wa Mau Mau waliposhambulia makazi ya Uingereza, na kusababisha hofu miongoni mwa walowezi weupe na kuishitua serikali mjini London.
"Tumekubaliana kumaliza suala hili nje ya mahakama," alisema mwanasheria wa Kenya Paul Muite, mshauri wa wapiganaji wa vita vya Mau Mau wanaodai fidia.
"(Maelewano) yamehusisha kila mtu na ushahidi wa kutosha wa mateso. Na idadi hiyo ni takribani 5,200," alisema, akikataa kuzungumzia ukubwa wa malipo hayo.
Tangazo rasmi katika malipo hayo linatarajiwa kutolewa mapema leo Alhamisi. Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza ilikataa kuzungumzia kuhusu ripoti kwamba malipo hayo yatafikia jumla ya Pauni za Uingereza milioni 14.
Hii itakuwa takribani Pauni za Uingereza 2,600 - au Shilingi za Kenya 339,560 - kwa kila mdai nchini humo ambako pato la taifa kwa kila mtu ni takribani Shilingi za Kenya 70,000.
Vikosi vya wapiganaji wa vita vya Mau Mau viliundwa miaka ya 1950 miongoni mwa watu wa kabila la Kikuyu la nchini Kenya. Walijitolea kuanzisha ghasia kupinga utawala wa Waingereza nchini humo.
Kamisheni ya Haki za Binadamu nchini Kenya imekadiria Wakenya 90,000 waliuawa au kulemazwa na 160,000 kushikiliwa mateka wakati wa mapinduzi hayo.
Serikali ya Uingereza ilijaribu kwa miaka mitatu kuzuia hatua za kisheria za wapiganaji hao wa vita vya Mau Mau katika mahakama kadhaa, wakipinga shutuma za utesaji kutoka waathirika hao wazee ambao wanawatuhumu wakoloni hao wa zamani wa Kenya kwa kutumia mbinu za kisheria kupambana na kesi hiyo.
Caroline Elkins, profesa wa historia wa Harvard ambaye alisimama kama shuhuda katika kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka 2009, alisema malipo ya fidia yatakuwa ya kwanza ya aina yake kwa Himaya ya Uingereza.
Uingereza mwanzoni ilisema kwamba kuwajibika kwa matukio wakati wa vita vya Mau Mau vilivyopitia nchini Kenya kabla ya Uhuru wake mwaka 1963, malumbano ambayo mahakama za London ilitupilia mbali.
Serikali hiyo kisha ilisema madai hayo yaliletwa baada ya muda wa mwisho wa kisheria. Lakini hukumu ya jaji ya Oktoba alisema kulikuwa na ushahidi wa filamu fupi kufanya uwezekano wa mashitaka ya haki.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

Trending Articles