Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

BINTI ASIMULIA BISKUTI ZILIVYOMWOKOA SIKU 17 CHINI YA KIFUSI CHA JENGO...

$
0
0
KUSHOTO: Reshma Begum akiwa kitandani hospitalini. KULIA: Jengo hilo lilipokuwa likiporomoka huku watu wakishuhudia.
Mwanamke ambaye aliokolewa baada ya siku 17 kutoka chini ya kifusi cha jengo la kiwanda cha nguo nchini Bangladesh amesimulia jinsi alivyookolewa kwa biskuti na chupa ya maji.

Reshma Begum ameishangaza nchi yake na dunia nzima pale alipochomolewa kutoka kwenye kifusi bila majeraha yoyote makubwa.
Reshma, ambaye ana umri wa miaka 19, alisema hayo siku jengo hilo lilipoanguka, aliharakisha kazini na hakubahatika kupata kifungua kinywa.
Badala yake, akanunua pakiti ndogo nne za biskuti akiwa njiani kuelekea kazini.
Ulikuwa uamuzi ambao uliokoa maisha yake - kwa jinsi alivyopangilia mlo wake huo kwa zaidi ya wiki mbili zilizofuata.
Wokovu wake - ambao ulirushwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa - ulisababisha kusimama kwa shughuli zote katika mji mkuu wa nchi hiyo, Dhaka, huku watu wakiacha kufanya kazi na kukusanyika kwenye televisheni zao.
Hivi karibuni, Reshma aliwaeleza wafanyakazi wa hospitalini hapo na waokoaji wake kwamba aliishi kwa kutegemea biskuti hizo na chupa za maji katika siku 15 za kwanza - huku akiwa amelala chali ndani ya uvungu katika jengo hilo lililoporomoka la Rana Plaza katika eneo la Savar la mjini Dhaka.
Inaaminika chupa hizo za maji zilizookoa maisha yake zilimfikia baada ya kuwa zimerushwa chini na waokoaji kupitia tundu moja. Waokoaji hao walielekezwa kutupa chupa hizo chini kupitia kila tundu na mvungu walioukuta - kwa matumaini wote walionaswa chini yake yanaweza kuwafikia.
Reshma - ambaye anaishi peke yake katika chumba alimopanga huko Savar - alisema kwamba pale jengo hilo la ghorofa nane lilipoanguka, alikuwa kwenye ghorofa ya tatu.
Aliweza kukimbia chini katika ghorofa ya pili lakini alinaswa katika mvungu. Mvungu huo ulikuwa mkubwa vya kutosha kwake kujigeuza na kulikuwa na hewa ya kutosha.
Lakini nywele zake zikanaswa chini ya nguzo, hivyo alilazimika kusukuma nguzo ili kuweza kujinasua.
Akiendelea kupata nafuu katika Hospitali ya Kijeshi huko Savar, Reshma alisema: "Hakuna yeyote aliyenisikia. Ilikuwa inatisha mno. Sikuwahi kufikiria kama ningeweza kuona jua tena."
Mshonaji huyo wa kike sasa ana matatizo ya kukosa usingizi usiku, na mara kwa mara huvuta mkono wa nesi kufuatia hofu ya mashambulio hayo.
Kanali Azizur Rahman, daktari mwanajeshi katika hospitali hiyo, alisema: "Hatutaki kumbukumbu hizo kumtafuna sasa, hivyo haturuhusu yeyote kumuuliza chochote.
"Kwa sasa anapatiwa vyakula vya rojorojo."
Imebainika kwamba familia ya Reshma ilifahamu kuwa yu hai baada ya kutazama zoezi la uokoaji kwenye televisheni.
Mama yake Zobeida Begum, ambaye yuko katika umri wa miaka ya 60, alisema: "Sikuweza kuamini pale nilipomuona akiwa hai hospitalini."
Dada yake Asma alisema: "Tumempata tena wakati tukiwa tumepoteza matumaini ya kumpata akiwa hai."
Walisema walikuwa wakikesha kwa ajili ya mshonaji huyo wa kike, ambaye anatokea vijijini katika wilaya ya Dinajpur, maili 170 kaskazini mwa Dhaka.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

Trending Articles