Moto wa ajabu umezuka ghafla na kuteketeza mali zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghala la vifaa vya ujenzi na umeme lililopo maeneo ya Tegeta Kibaoni, Wilaya ya Kinondoni.
Moto huo uliozuka bila chanzo chake kujulikana, umejirudia kwa mara ya pili, baada ya mara ya kwanza ulipozuka mwaka jana tarehe, muda na mwezi kama huu na kuteketeza mali bila mafanikio ya kuokoa kitu chochote.
Wananchi walioshuhudia moto huo wamesema kwa nyakati tofauti kuwa, kuna uwezekano chanzo cha moto huo kikawa ni baina ya wamiliki wenyewe wa eneo hilo kutokana na kujirudia kwa tukio hilo muda na siku zinazofanana.
Wakati moto huo ukiendelea kuwaka, wafanyakazi na wahusika wa eneo hilo walikimbia kwa kile kilichoelezwa ni kuchanganyikiwa.
Katika eneo la tukio, wakati wananchi na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiendelea na juhudi za kuuzima moto huo, askari polisi mmoja aliyekuwepo eneo hilo kwa ajili ya usalama wa raia alifanya tukio la kushangaza.
Askari huyo aliingia kwa ujasiri ndani ya chumba kilichokuwa kinafuka moshi badala ya kuokoa mali iliyokuwa ikiteketea, alionekana akichukua mfuko unaodaiwa ilikuwa ni pochi yenye fedha ndani yake na kutokomea nayo kusikojulikana.
"Polisi kaja katufukuza kisha kaingia ndani akachukua pochi na kuondoka huku akitufukuza kwa ukali," alisema shuhuda aliyemuona polisi huyo ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Wakazi na mashuhuda wa tukio, akiwemo mwandishi ni miongoni mwa watu walioshuhudia moto kama huo ukizuka eneo hilo mwaka jana. Hata hivyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa kwa ajali hiyo na thamani ya mali iliyoteketea haijajulikana.