Shirika lisilo la serikali linalotetea haki za wanawake na watoto la House of Peace limeombwa kufufua huduma za makazi walizokuwa wakizitoa kwa wanawake na watoto wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuwa mahitaji bado ni makubwa.
Huduma za makazi katika shirika hilo zilisitishwa mwaka jana 2013 kutokana na shirika kukabiliwa na uhaba wa fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli hizo.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki alioa ombi hilo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na watendaji wa shirika hilo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake aliyoifanya kwa asasi na mashirika yanayotoa huduma ya sheria kwa jamii.
“Angalieni ni namna gani mnafufua huduma hiyo... mahitaji ni makubwa na serikali itashirikiana nanyi kuona ni namna gani ya kufanya ili kama kuna uwezekano wa kupata fedha kidogo,” alisema Kairuki.
Kadhalika aliwashauri kuangalia namna ya kufanya harambee kuwezesha kupata fedha zitakazosaidia kuendesha utoaji wa huduma pamoja na kuanzisha miradi endelevu itakayowaokoa kiuchumi.
Awali akizungumza, Mratibu wa House of Peace, Perusi Makame alisema idadi ya wanawake na watoto waliopatiwa hifadhi ya muda kuanzia Januari 2012 hadi Juni 2014 ni 901 ambao walikumbwa na mikasa ya vitendo vya ukatili.