Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi ametangaza mlipuko wa ugonjwa wa kichaa cha mbwa na kutaka mamlaka husika kuhakikisha wanadhibiti hali hiyo.
Dk Nchimbi alisema hayo kwenye mkutano wa maandalizi ya Nanenane kwa Kanda ya Kati.
Katika mkutano huo, aliagiza maofisa husika kusambaza habari hizo kwa wananchi na mbwa wote watakaonekana kuzurura kuuawa.
"Mbwa ni lazima wafungiwe ndani na wale watakaonekana wanazurura ni lazima wauawe kuepuka kusambaza ugonjwa huo iwapo wanao," alisema.
Mkuu huyo wa mkoa alikuwa anathibitisha taarifa za Mganga Mkuu wa mkoa ambaye alisema kwamba kila siku kuna wastani wa watu 10 hufikishwa hospitalini hapo wakiwa wameng’atwa na mbwa.
Mkuu wa mkoa amesema kwamba kutokana na takwimu zilizopo ambazo ni watu takribani kumi kwa siku, hali si nzuri na kila anayehusika ni lazima achukue hatua.
Ofisa anayeshughulikia chanjo wa mkoa wa Dodoma, Paul Mageni amesema kwamba wastani wa wagonjwa kwa wiki kwa sasa ni 60.
Dk Mageni alirudia mwito wa Mkuu wa Mkoa na kusema ipo haja ya kukabiliana na tatizo hilo ili kulitokomeza.
Mapema, Dk Nchimbi alisema kwamba mbwa huwekwa kwa sababu za ulinzi na hivyo ni lazima wabaki katika makazi yao wanayolinda na wale wanaozurura ni lazima wauawe.
Kichaa cha mbwa ni ugonjwa unaosababisha kasoro katika ubongo wa mwanadamu na mbwa ambaye anayeumwa na mbwa mwenye ugonjwa huo baada ya siku kadhaa anakuwa na homa na tabia zinazofanana na mbwa, ikiwa ni pamoja na kubweka na kuogopa maji.