Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4652
↧

MOTO WATEKETEZA NYUMBA NA MADUKA DAR

$
0
0
Nyumba moja imeteketea kwa moto na nyingine vyumba viwili wakati moto huo ulipozuka ghafla kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam juzi.
Katika tukio la kwanza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema moto uliteketeza nyumba moja yenye vyumba 12 eneo la Mwananyamala A juzi saa 5.30 asubuhi.
Wambura alisema nyumba hiyo inamilikiwa na Siasa Abdallah (45) na kwamba hakuna madhara kwa binadamu ila vyumba vitatu ndivyo vilivyoteketea ambavyo ni maduka na kwamba ulianzia katika duka la vifaa vya ushonaji. Alisema chanzo cha moto huo hakijafahamika wala thamani ya mali iliyoteketea.
Katika tukio jingine, moto ulizuka eneo la Keko Magurumbasi, wilayani Temeke kwenye nyumba ya Simon Lucas (58) yenye vyumba 10 ikisadikiwa chanzo ni hitilafu ya umeme katika nguzo ya jirani na nyumba hiyo.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Engelbert Kiondo alisema moto huo ulizuka saa sita mchana na vyumba viwili viliteketea pamoja na mali zote zilizokuwemo ndani ya vyumba hivyo.
↧

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4652

Latest Images

Trending Articles