Jeshi la Polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi kutuliza ghasia zilizoibuka baina ya wakazi wa eneo la Bahari-Motors, Kijitonyama, wilayani Kinondoni jijini hapa.
Ghasia hizo zilitokana na kuchukuliwa kwa magari ambayo yalikuwa yameegeshwa katika gereji iliyopo eneo hilo. Hali hiyo ilisababisha wafanyabiashara wa eneo hilo kufunga maduka yao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi jana, wananchi hao walisema mara kwa mara Polisi hao wamekuwa wakifanya operesheni hiyo.
Mfanyabiashara Mussa Bakari alisema hivi karibuni Polisi walifika eneo hilo na kubeba magari yaliyokua yameegeshwa nje katika ukuta wa gereji hiyo.
Alisema baada ya kuchukuliwa kwa magari hayo, yalipelekwa kituo cha Polisi na baada ya wamiliki kuyafuatilia, walitozwa fedha nyingi.
Hivyo, hatuoni sababu ya kuchukuliwa magari yetu kwa sababu tangu zamani tulikuwa tukiegesha magari yetu hapa na baada ya kazi yanaingizwa ndani ya gereji,” alisema Bakari.
Mkazi mwingine, Ramso Maige alisema watu wamechoshwa na vitendo vinavyofanywa na askari visivyo shirikishi ndiyo maana wameamua kufanya fujo.
Mwandishi alishuhudia wananchi waliwarushia mawe Polisi nao wakiwatuliza kwa mabomu ya machozi kurejesha amani.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema hana taarifa ya ghasia hizo lakini alisema jeshi limekuwa likifanya operesheni Kinondoni kila siku katika maeneo tofauti.