Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4550

WIZARA YASISITIZA PROGRAMU YA KIFUNGO CHA NJE

$
0
0
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Idara ya Huduma kwa Jamii imesema ili urekebishaji wa wahalifu chini ya programu ya kifungo cha nje ufanikiwe, Serikali ichukue hatua za makusudi kueneza utekelezaji wa sheria ya huduma kwa jamii kwa nchi nzima.
Kwa kufanya hivyo, kunawezekana nusu ya wahalifu wote wakawa kwenye adhabu mbadala ya kifungo kama inavyobainishwa katika programu za huduma kwa jamii, Bodi ya Parole  na Probesheni endapo zitafanya kazi ipasavyo.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Jamii, Fidelis Mboya alisema hayo wakati akizungumza na gazeti hili jana, Dar es Salaam na kuongeza kuwa programu ya kifungo cha nje kimsingi ni ya kuendeleza sekta ya urekebishaji wa wahalifu.
Mboya alisema kwa utekelezwaji wa sheria hiyo malengo ya kupunguza gharama za uendeshaji magereza yataonekana, kadhalika msongamano wa magerezani utapungua na uzingatiaji wa haki za binadamu utaimarishwa katika maeneo hayo na kwenye jamii.
“Jamii itafaidika kwa huduma wa wahalifu na urekebishaji wa wahalifu utaboreshwa na viwango vya kurudia uhalifu vitashuka,” alisema Mboya.
Alitolea mfano wa nchi ya Kenya kuwa kwa sasa ndiyo  nchi ya Afrika inayofanya vyema zaidi katika matumizi ya adhabu mbadala ya kifungo, kwa kuwa na asilimia 50 ya wahalifu wote wa nchi hiyo kwenye adhabu nje ya magereza.
Aliongeza kuwa nchini humo Idara ya Probesheni na Huduma kwa Jamii, ina maofisa probesheni zaidi ya 600 waliotapakaa nchi nzima, ambazo kwa pamoja wanasaidia kupunguza msongamano wa mahabusu magerezani kwa kuepusha vijana na watoto kupelekwa magerezani.
Mboya alisema pia wanasaidia kusuluhisha migogoro katika jamii na kuepusha kufunguliwa kwa mashtaka mengi katika mfumo wa haki jinai.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4550

Trending Articles