Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe anatarajia kwenda nchini India ili kutoa shukrani kwa Serikali ya nchi hiyo pamoja na kuishawishi kupanua ufadhili na mikopo yake katika miradi ya maji nchini Tanzania.
Katika ziara hiyo, waziri huyo ataongozana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwasa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mbogo Futakamba, Mkurugenzi wa Uratibu Programu Joseph Kakunda pamoja na Mkurugenzi wa Huduma ya Maji Mijini Justus Rwetabula.
Akizungumza ofisini kwake jana, Mkurugenzi wa Uratibu Programu Wizara ya Maji, Joseph Kakunda, alisema lengo la safari hiyo ni kutoa shukrani kwa Serikali ya India, kuelezea mwenendo wa miradi ya maji inayotekelezwa na makandarasi wa India na kuiomba Serikali hiyo kupanua wigo wa misaada yake katika sekta ya maji nchini.
Katika ziara hiyo, Waziri Maghembe na msafara wake watakutana na Waziri wa Rasilimali za Maji wa India na viongozi wa juu wa wizara hiyo nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa wizara hiyo, Athuman Sharif, Profesa Maghembe pia anatarajiwa kukutana na viongozi wakuu wa Kampuni ya ujenzi ya WAPCOS kwenye makao makuu ya kampuni hiyo.
Alisema pia msafara wake utakutana na viongozi wa juu wa Wizara ya Fedha wa India pamoja na Idara ya Mikopo kwa nchi zinazoendelea.
Alisema baada ya hapo msafara huo utakutana na Uongozi wa Mamlaka ya Majisafi jijini New Delhi kwa ajili ya kupata uzoefu wa namna Mamlaka za maji za miji zinavyoendeshwa.
Sharif alisema msafara huo unatarajiwa kurudi Dar es Salaam Julai 19, mwaka huu na kuendelea na shughuli nyingine za kulijenga Taifa.
Serikali ya India imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Tanzania katika sekta ya maji kwa miaka mingi sasa. Ushirikiano wao umeanza tangu mwaka 1975 kwa kuwajengea uwezo wahandisi wa maji nchini.
Kwa sasa India inafadhili miradi kadhaa ya maji nchini ukiwemo mradi wa maji wa Chalinze na upanuzi wa mradi wa maji wa Ruvu Juu chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).