Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI), kimeandaa mikakati ya kuyafikia makundi mengi zaidi katika utoaji wa huduma yakiwemo makundi ya watu wanaofanya biashara ya ukahaba.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama hicho, Lulu Ng'wanakilala (pichani) alisema, chama hicho kikiwa kinasherehekea mika 55 tangu kuanzishwa kwake kimekuwa kikitoa huduma za uzazi wa mpango kwa muda mrefu lakini kwa sasa kimeongeza huduma zaidi.
“Pamoja na kutoa huduma za uzazi wa mpango, kwa sasa pia tunatoa huduma za magonjwa ya zinaa, virusi vya Ukimwi na saratani ya kizazi ambayo ni tatizo kubwa kwa wanawake wengi kwa sasa,” alisema.
Alisema kwa sasa wanahudumia vijana zaidi ambao ndiyo walengwa wakubwa lakini pia wamepanua huduma zao ili kuwafikia watu wanaouza miili yao pamoja na madereva wa bodaboda.
Alisema bado Tanzania ipo nyuma sana katika masuala ya kuzuia vifo vinavyotokana na uzazi na hali hiyo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na uhaba wa huduma za uzazi wa mpango pamoja na ndoa za utotoni.
“Wakati malengo ya serikali yakiwa kufikia asilimia 60 mwaka 2015 lakini hadi sasa ni asilimia 27 tu ya Watanzania wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango na asilimia 7 wanatumia njia za kienyeji…Tunataka kuwahamasisha wanaume nao watumie huduma za uzazi wa mpango,” alisema.
Pia alisema wataboresha huduma zaidi katika vituo vyao mikoani ili kuhakikisha wanawafikia Watanzania wengi zaidi katika huduma wanazozitoa.