Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

TRA WAOMBA NGUVU ZA WASANII KUFANIKISHA UDHIBITI

$
0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imewataka  wasanii  kushirikiana nao  katika operesheni waliyoanzisha  kuhakikisha wanadhibiti watu wanaodurufu kazi  zao ili ziweze kurudi kwenye mstari na kupata mapato.
Aidha, imesema TRA inataka kuboresha mfumo wa utoaji stampu ziwe za kielektroniki na kuachana na za karatasi ili ziwe bora zaidi katika  bidhaa zote.
Hayo yalibainishwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa tafiti na sera wa (TRA), Tonedeus Muganyizi katika Maonesho ya 38 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere katika barabara ya Kilwa  maarufu kama Sabasaba.
Alisema mwitikio wa wasanii bado uko chini hasa wasanii wa muziki katika kupambana na watu hao  kwani hawajawa na mwamko wa  kuweka kazi zao stampu lakini wasanii wakubwa wa filamu wamekuwa na mwamko na uelewa juu ya suala hilo.
Alisema kwa kuzingatia suala hilo imeanza operesheni ya kukamata watu wanaodurufu kazi za wasanii na kuziuza mitaani kwa bei nafuu ambazo hazina stampu ili kukomesha tatizo hilo.
Alisema kazi za wasanii zimekuwa zikidurufiwa sana na kuuzwa mitaani  kwa bei nafuu na kuacha kununua CD ambazo zimethibitishwa na  Cosota na kupewa hatimiliki ambazo zinatambulika kisheria na kubandikwa stampu na mamlaka hiyo.
Alisema kuwa tayari wameshakamata  mitambo mbalimbali ambayo inatumika kudurufu kazi hizo maeneo ya Kariakoo na watu wanaoziuza  na kuwachukulia hatua ili waweze kumaliza tatizo hilo.
Hata hivyo alisema msanii yeyote lazima apitie Basata na Cosota  ili aweze kupewa hati miliki baada ya hapo  anapeleka kazi zake TRA ili ziweze kuwekwa stampu ambazo zitakuwa halali kuuzwa sokoni.
Pia alisema  wameshaunda timu ambayo imehusisha watu kutoka TRA, Cosota  na Basata ambao wanafanya operesheni hiyo katika maeneo mbalimbali ili kubaini watu wanaouza CD ambazo hazina stampu kwani hali hiyo inakosesha wasanii wengi mapato.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

Trending Articles