Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

SIDO YAANIKA UBUNIFU WAKE KUKUZA KILIMO

Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO), limesema dhamira kuu katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam ni kutoa muamko kwa wajasiriamali kwa kuonesha utaalam katika suala la ubunifu kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya kilimo.
Shirika hilo limeeleza kuwa wamejitahidi kuandaa mashine bora zitakazosaidia kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa mazao ya kilimo na ufugaji, ambapo Mjasiriamali ataweza kunufaika endapo ataweza kuzitumia.
Meneja Masoko wa SIDO, Henrick Mdede, alisema kwenye Viwanja vya Sabasaba jana kuwa ubunifu ndio siri kuu ya mafanikio kwa mjasiriamali, kwa sababu itawasaidia kuweza kupata soko la uhakika na lenye manufaa maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
“SIDO inasisitiza kuwa wajasiriamali wahakikishe bidhaa zao zinakuwa na ubora unaokidhi mahitaji ya soko wanalolidhamiria ikiwemo kutumia mistari ya utambuzi 'Barcode',” alisema Mdede.
 Alisema wajasiriamali hao wanatakiwa waelewe kuwa biashara yo yote inahitaji uelewa wa soko. Alisema anaamini wajasiriamali na wananchi wote kwa ujumla wakija kwenye maonesho haya ya biashara, watajifunza mengi ikiwemo kujifunza uelewa huo, ambao ni muhimu sana kwa maendeleo ya mfanyabiashara.
Alisema wajasiriamali wengi nchini ni kuwa waoga wa kujaribu kwa kuhofia kupata hasara katika jambo ambalo halina tija kwa biashara yake.
SIDO inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa inamsaidia mjasiriamali kutoka kwenye ngazi ya chini kwenda nyingine kimaendeleo, hivyo wajasiriamali wajitahidi kuwa pamoja na taasisi hiyo.
Ndede alisema SIDO wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwasaidia wafanyabiashara wadogo nchini kusimama na kujitegemea ambapo katika maonesho ya mwaka huu wameweza kuandaa mashine nyingi ikiwemo ya kuvunia mpunga, kubangulia kahawa, kutotolesha mayai ya kuku na kuchuja mchanga kwa ajili ya shughuli za uchimbaji wa madini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

Trending Articles