Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

ZEC YAHIMIZA WANAWAKE KUJITOKEZA KUGOMBEA UONGOZI

$
0
0
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetaka wanawake kushiriki katika mchakato wa uchaguzi kuanzia ngazi mbali mbali na kugombea katika nafasi za juu za uongozi katika vyama vya siasa.
Imeelezwa kuwa hatua hiyo itaimarisha demokrasia ya vyama vingi na mchango wa jinsia hiyo kuonekana kwa wananchi.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa ZEC,  Jecha Salum Jecha  alipofungua semina iliyowashirikisha wadau mbalimbali, ikiwemo vyama vya siasa kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu.
Alisema wanawake ni miongoni mwa makundi ambayo hayashirikishwi ipasavyo, ingawa mchango wao katika uchaguzi ni mkubwa.
“Katika mkutano huo tumeweka mikakati mbalimbali ikiwemo ushiriki mkubwa wa wanawake katika uchaguzi mkuu na kuona wanashirikishwa kikamilifu kama ni sehemu ya wadau,” alisema.
Alitaka wanawake kwa ujumla, kujitokeza kwa wingi kushiriki katika nafasi za uongozi kuanzia uchaguzi wa Serikali ya Mitaa, Ubunge na Uwakilishi.
Awali, Mratibu wa Kitengo cha Uchaguzi katika Kamisheni ya Bara la Afrika, Shumbana Amani Karume, alisema wakati umefika kwa wanawake kupewa kipaumbele katika vyama vya siasa, kushiriki katika nafasi mbali mbali za uongozi.
Alisema mchango wa wanawake katika demokrasia ya Afrika ni mkubwa, lakini kwa bahati mbaya hawajashirikishwa kikamilifu katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Mmoja wa washiriki katika mkutano huo, Khadija Juma alisema vyama vya siasa, vimekuwa vikiwatumia vibaya wanawake kama ngazi ya kupata nafasi za uongozi.
“Semina hii imetusaidia sana sisi wanawake kuweza kuzitambua haki zetu na kushiriki kikamilifu katika demokrasia ya vyama vingi kufikia ngazi za maamuzi', alisema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles