Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

WAOMBA USHIRIKIANO WA RAIA KUDHIBITI UHAMIAJI HARAMU

$
0
0
Idara ya Uhamiaji imewataka wananchi kutoa taarifa pale wanapoona kuna wahamiaji haramu wanaishi katika mazingira yao au wanaishi bila kibali hapa nchini ili wachukuliwe hatua.
Ofisa Uhusiano wa Idara ya Uhamiaji, Tatu Burhani,alisema hayo jana katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayofanyika katika  barabara ya Kilwa katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba. 
Alisema kuwa  wananchi wanatakiwa kutoa taarifa  za wageni wanaowaona katika maeneo yao ya makazi au waliowatilia shaka ili kubaini kama wapo kisheria hapa nchini.
"Kuna wageni mbalimbali wanaingia hapa nchini kupitia barabara za  panya hivyo ni vyema wananchi wakashirikiana na  Uhamiaji ili kuwafichua na sheria ichukue mkondo wake,"alisema Burhani.
Pia alisema kuna baadhi ya wageni wanaoingia hapa nchini kihalali kwa lengo la kutembea  lakini  baada ya muda utawakuta anafanya kazi  sehemu hao ni wahamiaji haramu kwani  kibali alichopewa ni cha  kutembea tu  hivyo wananchi wakibaini  watu kama hao watoe taarifa.
Hata hivyo alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali moja ikiwa ni ukubwa wa mipaka ya Tanzania hivyo  kushindwa kuwadhibiti maeneo yote kutokana na wageni wengine hupitia njia za panya kuingia nchini.
Pia alisema wanakabiliwa na changamoto za kijamii kama  zinazotokana na mwingiliano wa watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine katika nchi tunazopakana nazo.
Alisema kutoka na hali hiyo  wamejipanga kuimarisha  doria, misako na oparesheni mbalimbali ili  kuwasaka wahamiji haramu wanaoishi hapa nchini kinyume na taratibu.
Pia alisema wanaongeza mafunzo kwa watumishi wa idara hiyo ili kubaini mbinu mbalimbali wanazotumia wahamiaji haramu kuingia hapa nchini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

Trending Articles