Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4630

MWAMBUNGU AZIBANA HALMASHAURI RUVUMA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu amezitaka halmashauri za wilaya na halmashauri za Manispaa,  kurejesha vijijini asilimia 20 ya mapato yanayotokana na ushuru ili yafanye kazi za maendeleo.
Mwambungu alisema hayo katika Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea. Kikao hicho kilijadili mapato na matumizi ya halmashauri hiyo.
Mwambungu alisema halmashauri nyingi, zimejenga tabia ya kukusanya ushuru na kusahau kuwarudishia wale waliozalisha.
Pia, Mkuu  huyo wa Mkoa alizitaka halmashauri za mkoa wa Ruvuma, kuhakikisha mapato yanayokusanywa yanapelekwa benki.
Katika kikao hicho, madiwani wa Halmashauri ya Songea walilalamikia vitendo vinavyofanywa na Serikali vya kukaimisha madaraka na kwa kuwaacha makaimu kwa muda mrefu.  Walisema hali hiyo inazorotesha maendeleo.
Aidha, halmashauri ya Wilaya ya Songea ilisema inakabiliwa na changamoto ya kutolipwa fedha za ushuru wa mazao, zinazokusanywa na Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA).
Mpaka sasa Halmashauri hiyo inaidai NFRA jumla ya Sh milioni 739, ambazo zilikuwa za ushuru wa msimu wa mwaka jana 2012/2013.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma aliahidi kusaidia kufuatilia ili fedha hizo zipatikane.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4630