Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi anatarajiwa kufungua kongamano la Majeshi ya Nchikavu ya nchi za Afrika Mashariki lenye lengo la kujadili changamoto zinazowakabili.
Kongamano hilo linalotarajiwa kukutanisha wataalamu zaidi ya 300 linatarajiwa kufanyika siku mbili mfululizo kuanzia Julai 15 na 16 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kongamano la maonesho ya Majeshi ya Nchikavu Afrika ya Mashariki, Tracey –Lee Zurcher alisema, nchi za Afrika Mashariki zina shauku kubwa ya kutaka kujilinda.
“Nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki zina shauku kubwa ya kujilinda, sio tu kwa kuwa na maarifa bali pia kuwa na zana ili kuimarisha miundombinu ya ulinzi wao.
“Kutokana na misukosuko ya kisiasa wanayokumbana nayo sasa kwa upande wa uharamia na vikosi vya waasi, serikali hizi zinatakiwa kuongeza kwa kasi uwezo wa ulinzi wa nchi kavu pamoja na uwezo wa misaada ya kibinadamu,” alisema Zurcher.
Alisema maonesho kama vile ya Majeshi ya Nchi kavu Afrika na Ulinzi wa Majini Pwani ya Afrika, imeonesha kuwa iko haja ya kuwa na ubora wa hali ya juu kimikakati na kiufundi kwa pamoja katika ngazi za kikanda.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, Afrika ya Mashariki kwa sasa ndio imekuwa eneo ambalo lina fursa kubwa katika sekta ya ulinzi. Na hii ni kutokana na takwimu kuonesha bajeti za ulinzi katika ukanda huu zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 13.6 kwa mwaka, ambayo ni mara tano zaidi ya wastani wa sekta hiyo.
Alisema bajeti kwa upande wa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara imeongezeka kwa asilimia 18 mwaka 2013 na matumizi kwa upande wa ulinzi yanatarajiwa kuzidi dola za Marekani bilioni 46 kufikia mwaka 2018. Takwimu hizo zote zinaashiria kuwa kuna fursa kubwa katika ukanda huu kwa wasambazaji wa zana katika sekta ya ulinzi.
Mkutano na Maonesho ya Majeshi ya Nchi kavu Afrika ya Mashariki na Ulinzi wa Majini katika Pwani ya Afrika yatakutanisha maofisa zaidi ya 300 wa kijeshi, wadau wa serikali, na wataalamu katika maeneo ya sekta ya ulinzi na usalama.
“Maonesho haya yatajumuisha wasambazaji zaidi ya 30 wanaongoza katika upande wa zana za kiulinzi ikiwemo; Denel, Otokar na Armscor, ambao wanaleta kampuni 10 za ulinzi na usalama kutoka Afrika Kusini kuonesha ufumbuzi wao kwa upande wa soko la Afrika Mashariki,” alisema Zurcher.