Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) imeanzisha fao la kifo kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi, ambapo pia wategemezi wao wanne waliopo nchini, watanufaika nalo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa wateja wa shirika hilo, Eunice Chiume (pichani) alisema hayo jana katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema watanzania hao walio nje ya nchi, wanatakiwa kulipa dola za Marekani 300, ambayo ni sawa na Sh 500,000 kwa mwaka na kiasi hicho kitamwezesha anapofariki dunia, mwili wake kuletwa nchini pamoja na mtu mmoja wa kumsindikiza.
Alisema wameanza kutoa elimu kwa watanzania wa nchi za Uingereza na Marekani; na sasa wanaelekea China, ambako wameelezwa kuna watanzania wengi, kisha wataenda katika nchi nyingine duniani.
“Pia mchangiaji atachagua wategemezi wake wanne wanaoishi nchini watakaowezeshwa kupata mafao ya matibabu katika hospitali mbalimbali nchini,"alisema.
Alisema tangu waanze kutangaza fao hilo kwa watanzania wa nje ya nchi, kumekuwa na ‘kusuasua’, kutokana na gharama ndogo za uchangiaji huku gharama za usafirishaji zikiwa kubwa, ambazo ni zaidi ya dola za Marekani 10,000. Lakini, alisema tayari kuna Mtanzania aliyejiunga na kusafirishwa kwa muda mchache kupelekwa mkoani Kagera.
Chiume alisema changamoto waliyonayo sasa ni katika ulipaji wa fedha hizo, kwani umekuwa na gharama kubwa, lakini wanajipanga kuweza kutafuta mawakala, ambao watakuwa watanzania wenye shughuli maalumu nje ya nchi.