Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

WAKULIMA, WANUNUZI WACHAKACHUA PAMBA ILI KUONGEZA UZITO

$
0
0
Wakulima wa zao la pamba  na wanunuzi  wa zao hilo,  wamekuwa ni chanzo cha kudhoofisha zao hilo, hivyo kushindwa kuingia katika ushindani wa soko.
Imedaiwa kuwa baadhi ya wakulima wamekuwa wakiweka maji kwenye pamba, ili kuongeza uzito wa pamba, hasa pale  inapotangazwa  bei  ndogo ya pamba.
Pia, imedaiwa kuwa wanunuzi na wahasibu, nao hunyunyizia  chumvi au sukari, kwa lengo la kuongeza uzito wa pamba ili kupata faida.
Hayo yalisemwa na baadhi ya wadau wa zao hilo  kutoka wilaya za Bariadi na Itilima mkoani Simiyu.
Walisema hayo katika mdahalo, ulioandaliwa na shirika lisilo la kiserikali  lenye kutetea masuala ya utawala bora, uwajibikaji na  kilimo la ADLG, kwa ufadhili wa Jukwaa la  mashirika yanayojihusisha na kilimo (ANSAF).
Mmoja wa wadau hao kutoka wilayani Bariadi, Moses Sosoma  alisema pamba  inalimwa Bariadi,  sio kwa lengo la kibiashara, bali linalimwa ili  kuondoa changamoto ndogo kwenye kaya.
Pia, alisema baadhi ya wakulima katika wilaya hiyo, wamekuwa wakidiriki kuchanganya pamba na maji, chumvi na sukari kwa lengo  kuongeza uzito. Alisema vitendo hivyo vimefanya zao hilo, kukosa thamani.
“Kila msimu wakulima wamekuwa wakilalamikia  ubora wa pamba kutokana na kushuka kwa  bei. Kinachotakiwa kwa sasa ni  wakulima waandaliwe kuanzia ngazi  ya chini kwa kuelimishwa ubora unaotakiwa  ili kupata bei nzuri?” alisema Diwani wa Kata ya  Bariadi, David Sendo.
Mwenyekiti wa Halmashauri  ya Wilaya ya Bariadi, Bahati Magamula alisema kumekuwepo na changamoto nyingi kwenye kilimo cha zao la pamba katika mkoa wa  Simiyu, unaoongoza kwa uzalishaji wa zao hilo nchini. Alisema mkoa huo unazalisha asilimia 40 ya pamba yote inayolimwa nchini.
Alisema hakuna ufumbuzi uliopatikana hadi sasa, kuhusu changamoto za zao hilo Alisema kila mwaka wamekuwa wakikaa vikao vingi, lakini wameshindwa kupata majibu huku wakulima wakizidi kuumia.
Mtafiti wa Kujitegemea  wa zao la pamba, Geofrey  Chambua  alisema kuanzia mwaka  2005 hadi 2009, uzalishaji wa zao wa pamba ulikuwa mkubwa  na liliweza kuingiza Taifa Sh bilioni 92, hivyo kuwa zao la kwanza katika kuingiza pato kubwa.
Lakini, baada ya hapo, uzalishaji umeendelea kushuka, ambapo katika musimu wa mwaka 2012/13, zilizalishwa tani 351,151 na mwaka 2013/14 uzalishaji ulikuwa tani 246,767.
“Kushuka  kwa bei ya pamba, kulitokana na kuvurugika  kwa mfumo  msimu uliopita, ambapo bei ilikuwa shilingi 700  kwa kilo na sasa ni shilingi 750. Kinachochangia bei  hiyo ni kukosekana kwa viwanda vya ndani, ambavyo vingeleta ushindani katika soko. Kule Marekani  pamba yake ipo kwenye ushindani, kwa sababu nchi hiyo ina viwanda vingi. Pamba ya Tanzania ni ya mwisho duniani katika soko,” alisema  Chambua.
Mkurugenzi wa shirika  hilo,  Jimmy  Luhende alisema pamba  inayotoka shambani ni safi na  inavunwa kwa kutumia mkono.
Alisema changamoto kubwa  zilizojitokeza  ni gharama kubwa za uzalishaji, wakati kipato cha wakulima, wanachotumia katika kilimo  hicho, ni kidogo.
Alitaja changamoto zingine kuwa ni mbegu zinapopandwa kutochipua vizuri na baadhi ya dawa  za kuua wadudu kuwa feki.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

Trending Articles