Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amewataka maaskofu kujadili njia bora zaidi ya kusimamia maadili ya vijana, kufuatia nchi kukabiliwa na changamoto ya mmomonyoko wa maadili.
Alisema hayo jana katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka wakati akifungua mkutano wa Maaskofu wa Kanisa la Moravian Duniani, unaofanyika jijini hapa.
“Kuna kundi kubwa la waamini linalowategemea ninyi maaskofu kwa kuwapelekea habari njema za kiroho hivyo mnaweza kuisaidia serikali kujenga maadili mema mbele ya Jamii,” alisema.
Alisema kanisa likishirikiana na serikali, wanaweza kujenga Taifa lenye maadili na kupunguza changamoto ya kuwa na watu hususani vijana wasio na maadili, kwani watajengewa imani inayokwenda sambamba na matendo mema.
Alisema kazi ya kanisa ni kuwasaidia waumini na watu wote duniani, kuyajua matendo ya Mungu, kwani hiyo ndio njia mojawapo ya kuleta maendeleo na mahusiano mazuri kati ya serikali na madhehebu ya dini na wananchi.
Alisema madhehebu ya dini yamekuwa karibu na serikali kwa ajili ya kuleta maendeleo ya watu wake kupitia nyanja ya elimu, kilimo, afya, maji na makundi ya mahitaji muhimu.
“Natambua Moravian duniani kote inatoa huduma kwa jamii kupitia hospitali, shule, vyuo vikuu na hii inayotokana na kuijali jamii kimwili na kiroho,” alisema.
Alisema hapa nchini serikali inathamini mchango wao na kanisa litambue kuwa kwa kushirikiana na waumini, watapata maendeleo kwa haraka, kwani ukuaji wa kanisa hutegemea maendeleo ya waumini, kwani ndio wasimamizi wa miradi mbalimbali.
Mkutano huo unawakutanisha maaskofu 400 kutoka katika Mabara ya Ulaya, Asia, Afrika, Amerika ya Kaskazini na Kusini, una lengo la kushiriki na kuandaa utaratibu mzuri ili Dunia iwe mahali pazuri pa kuishi kwa amani na utulivu.