Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imesema unyanyapaa bado ni tatizo kubwa nchini, kuwezesha kufikia sifuri tatu mwakani, kama ilivyo katika mkataba wa Umoja wa Mataifa.
Kwa mujibu wa makubaliano ya kimataifa inatakiwa kufikia mwakani, kuwe hakuna maambukizi ya virusi vya Ukimwi, vifo vitokanavyo na Ukimwi pamoja na kutokuwepo na unyanyapaa.
Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti kutoka Tume hiyo, Dk Raphaeli Kalinga alisema hayo jana katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema ingawa Tanzania inaweza isifikie sifuri hizo tatu kama inavyoelekezwa, lakini nchi imefanikiwa katika kupunguza maambukizi mapya ya virusi hivyo na vifo vitokanavyo na ugonjwa huo, lakini changamoto imebaki katika unyanyapaa.
“Unyanyapaa bado ni tatizo kubwa kutokana na waathirika kunyimwa huduma mbalimbali na hata watu kujinyanyapaa wenyewe kwa kutokubali kupima huku suala la ukimwi likisababisha migawanyiko katika familia,” alisema.
Kalinga alisema kwa sasa nchi imejikita katika maeneo matatu kwa kuwekeza kwa vijana kuhakikisha hakuna maambukizi mapya kwa vijana, kuwekeza kwenye mikoa yenye maambukizi makubwa kama Njombe, Mbeya, Iringa.