Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

MAKANDARASI WASIO NA UWEZO KUPIGWA JEKI

$
0
0
Makandarasi nchini wanaoshinda zabuni mbalimbali za ujenzi lakini hawana uwezo wa kuwa na mashine za kisasa, watakodishwa mashine hizo na Kampuni ya Aydin Logistics.
Kampuni hiyo ya mwekezaji kutoka Uturuki, inawezesha wakandarasi hao kukodisha vifaa ili mradi wawe na barua inayoonesha kushinda zabuni aliyopata.
Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Hillary Keraryo, alisema hayo katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, ambapo wanatangaza mashine ya kisasa ya Hidromek kwa ajili ya ujenzi wa aina mbalimbali.
 Alisema watakaokodishwa mashine hizo, watachagua wenyewe kulipa kwa miezi sita hadi mwaka mmoja  kwa ajili ya kumkomboa mtanzania kuweza kufanya kazi za zabuni za ndani ya nchi ; na siyo kuwapatia wa nje ya nchi.
“Watanzania wanatakiwa kutumia fursa hii ya kujenga uhusiano huu kati ya Uturuki na Tanzania kwa kukodisha vifaa hivi vya kisasa kutoka Uturuki  bila kuwa na dhamana kubwa, kama zifanyavyo kampuni nyingine,”alisema.
Pia, alitaka kampuni ndogo za kukarabati miundombinu iliyoharibika kwa mvua, kama vile kampuni  zilizopo katika Manispaa, kukodisha vifaa hivyo kwa maendeleo ya nchi na wananchi wake.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

Trending Articles