Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete juzi alitembelea Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba' na kueleza kuwa amefurahishwa na juhudi zinazofanywa na wajasiriamali hasa wanawake.
Mama Salma alisema juhudi zinazofanywa na akinamama wajasiriamali, zinahitaji kupongezwa na kupewa msaada zaidi ili kuweza kupiga hatua kubwa.
Alisema bidhaa walizotengeneza, zinavutia watu wengi na hata akinamama wengi ambao hawajishughulishi na ujasiriamali, inawapa hamasa ya kufanya hivyo.
"Hongereni sana, juhudi mnazizoonesha ni kubwa sana, nimefurahi kuona bidhaa zenu ziko katika kiwango kizuri, ‘wanawake wakiwezeshwa wanaweza," alisema Mama Salma wakati akiwa kwenye banda la Mama Anna Mkapa la Fursa Sawa Kwa Wote(EOTF).
Aidha, akiwa katika banda la Pride, Mama Salma aliutaka uongozi wake kuendelea kuwasaidia na kuwawezesha akinamama ili waweze kufikia malengo yao.
Alisema kwa kuangalia Sabasaba ya mwaka jana na mwaka huu, na kadri miaka inavyokwenda mbele, akinamama wanazidi kuboresha bidhaa zao na kuleta ushindani kwenye soko.