Serikali imeshauriwa kusimamia na kutilia mkazo ipasavyo Sheria ya Maziwa ili kuzuia usambazaji holela na hivyo kusaidia uzalishaji wa maziwa katika viwanda nchini.
Usambazaji holela wa maziwa kwa kiasi kikubwa umesababisha kuathiri uzalishaji katika viwanda nchini, jambo linalofanya viwanda hivyo kuzalisha chini ya uwezo wao.
Ushauri huo ulitolewa na Meneja Masoko wa Kiwanda cha Maziwa cha Asas cha Iringa, Jimmy Kiwelu wakati akizungumza na mwandishi, ambapo alisema, mbali na usambazaji huo, pia ufugaji mdogo wa ng'ombe nao unachangia.
Alisema kiwanda chake kimeamua kuchukua jukumu la kuwaelimisha baadhi ya wafugaji juu ya umuhimu wa kufuga ng'ombe ili kupata maziwa ambayo wanaweza kuyauza kwa faida kubwa.
Kwa mujibu wa Kiwelu, kampuni yake imeamua kuongeza mashamba ili kuongeza uzalishaji wa maziwa na kuhakikisha kuwa maziwa yao yanamfikia kila mmoja.
"Bado usambazaji holela wa maziwa ni tatizo kwa kuwa unasababisha uzalishaji kuwa mdogo katika viwanda vyote nchini, lakini tunajaribu kukabiliana nalo kwa kuongeza mashamba tunayochukua maziwa," alisema Kiwelu.