Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

NYANDA ZA JUU KUSINI WAONGOZA MAAMBUKIZI MAPYA YA UKIMWI

$
0
0
Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imesema maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi nchini yamepungua hadi kufikia asilimia 5.1 kwa mwaka 2011/2012  ambapo asilimia 6.2 ni wanawake na asilimia 3.8 ni wanaume.
Taarifa hizo ni kutokana na utafiti uliofanywa na tume hiyo ambapo  Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka tume hiyo, Dk Jerome Kamwela alisema jana katika viwanja vya Sabasaba alipokutana na waandishi wa habari katika banda la TACAIDS kuwaelezea hali halisi ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi nchini.
“Tafiti zinaonesha kuwa Mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi ya virusi hivyo kwa asilimia 14.7 ambapo Iringa ina asilimia 9.1 ya watu walioathirika na  Mbeya ikiwa na asilimia 9. Mikoa yenye kiwango cha chini cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi ni Manyara na Kilimanjaro ikiwa na asilimia mbili ya maambukizi ya virusi hivyo,” alisema.
Akizungumzia changamoto ambazo TACAIDS imekuwa ikizipata katika ukusanyaji wa takwimu za watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini, Dk Kamwela alisema kuwa uhaba wa wataalamu, uhaba wa vyuo vinavyofundisha taaluma ya ufuatiliaji na tathmini pamoja na uhaba wa fedha kwa ajili ya kufuatilia na kutathimini hali halisi ya maambukizi ya Ukimwi nchini, vimekuwa vikizuia malengo ya kutokomeza Ukimwi nchini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

Trending Articles