Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4588

WATOTO 5,000 WAONDOLEWA KATIKA AJIRA MBAYA ZANZIBAR

$
0
0
Jumla ya watoto 5,000 wameondolewa katika ajira mbaya Unguja na Pemba ikiwemo za kugonga kokoto na kupasua miamba ya mawe ya kutengeneza matofali  katika mradi unaotekelezwa na Shirika la Save Children Fund Zanzibar.
Watoto 3,668 wamerudishwa shule baada ya kukimbia na kujikita katika ajira mbaya huku familia zao zikipewa fedha za kuendesha miradi ya kujikimu na kupunguza umasikini.
Ofisa mwandamizi wa mradi wa kupambana na ajira mbaya za watoto katika shirika hilo kwa Zanzibar, Jennifer Tavengerwei alisema hayo wakati alipozungumza na gazeti hili ofisini kwake mjini hapa.
Alisema mradi wa kupambana na ajira mbaya kwa watoto wa miaka mitatu ambao unafikia utekelezaji wake mwisho wa Septemba mwaka hii umepata mafanikio makubwa ikiwemo kuwarudisha shule watoto na kuziwezesha familia zao kujiendeleza kwa miradi wanayoitekeleza.
Alisema bado wazazi wanaendelea na tabia ya kuwatumikisha watoto wao ajira mbaya ambazo zimekuwa zikidumaza maendeleo ya watoto pamoja na kukosa baadhi ya fursa muhimu za msingi ikiwemo elimu.
Alisema hali ni mbaya zaidi katika kisiwa cha Pemba katika maeneo ya Mwambe na Micheweni ambapo watoto wanashiriki katika ajira ngumu za kukata miamba ya matofali yanayotumika kwa ajili ya kazi za ujenzi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4588

Trending Articles