Mbunge wa Chato, Dk John Magufuli ameasa wananchi kuepuka malumbano na kuweka mbele itikadi za vyama, badala yake washirikiane kujenga jimbo hilo.
Magufuli ambaye ni Waziri wa Ujenzi, alisema hayo jana katika mikutano yake ya kuhamasisha maendeleo katika kata za Kasenga, Ichwankima na Kachwamba wilayani Chato mkoa wa Geita.
“Ndugu zangu tufanye kazi kwa bidii, maendeleo hayaji hivi hivi, tuache malumbano na itikadi zetu za vyama ili tujenge jimbo letu vizuri,” alisema Waziri Magufuli.
Alisema Serikali ya CCM haina ubaguzi na ndiyo maana inapeleka maendeleo katika maeneo yote na hata yale yanayongozwa na wapinzani.
“Mnatakiwa kushirikiana na Serikali na siyo kubeza kama watu wengine wanavyofanya. Serikali yetu imefanya mambo mengi mazuri ya kuwaletea maendeleo,” alisisitiza.
Katika hatua nyingine, Magufuli alimtaka Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Peter Ngunula kuhakikisha kuwa ndani ya miezi miwili wananchi wa kata ya Kasenga wanapata maji .
“Mhandisi naomba baada ya miezi miwili wananchi hawa waanze kupata maji kama awali, na wananchi mtunze miundombinu ya maji haya ili tuweze kutatua kero hii kwa pamoja” alisema Waziri Magufuli.
Katika kusisitiza jambo hilo, Magufuli alichangia shilingi milioni moja zisaidie katika utatuzi wa kero hiyo ya maji.
Katika hatua nyingine, Waziri Magufuli aliwaahidi wakazi hao kuwa Serikali imeanza mchakato wa kuwaletea umeme na wajiandae na fedha kidogo ya Sh 27,000 kwa ajili ya uunganishaji.