Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

KIKWETE AMKARIBISHA MWANA MFALME WA JAPAN

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete amemkaribisha Ikulu, Dar es Salaam, Mwana wa Mfalme wa Japan, Prince Akishino pamoja na mkewe Princess Akishono.
Mwana Mfamle huyo ambaye anatembelea Tanzania, alifanya mazungumzo jana na  Kikwete.
Katika mazungumzo yao, Rais Kikwete alisema  Japan ni mshirika mkubwa na muhimu wa maendeleo ya Tanzania.
“Tunathamini sana mchango wenu katika maendeleo ya Tanzania na tunaendelea kuwashukuru sana. Ukizunguka nchini mwetu utaona kwa macho yako miradi mingi na mikubwa ambayo imejengwa ama inajengwa kwa msaada wa Japan,” alisema.
Rais Kikwete aliongeza: “Pamoja na ushirikiano huu. Bado tunaamini kuwa Japan inaweza kusaidia zaidi Tanzania hasa kwa kushawishi makampuni yake kuwekeza katika sekta binafsi. Ukipita mitaa ya Dar es Salaam, magari tisa kati ya 10 ni ya Kijapani. Ukiingia katika maduka ya vyombo vya elektroniki - televisheni, kompyuta, kamera, karibu kila kitu kinatoka Japan. Hali hii inathibitisha kuwa bidhaa vya Japan zina soko kubwa na zinaweza kuzalishwa hata hapa nchini na makampuni binafsi.”
Rais Kikwete pia aliitaka Japan, kuangalia jinsi gani inavyoweza kusaidia ongezeko la watalii kutoka Japan kuja kutembelea Tanzania kwa kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka huko hadi Tanzania na nchi nyingine za Afrika.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete alipokea hati za utambulisho wa mabalozi watatu, wanaowakilisha nchi zao nchini.
Mabalozi hao ni  Balozi wa Sri Lanka nchini, Dk Kana Kananathan,  Balozi wa Poland, Marek Kowski na  Balozi wa Romania, Julia Pataki.
Mabalozi hao waliwasilisha hati zao jijini Dar es Salaam jana  kwa rais Kikwete, ambapo pamoja na mambo mengine walipokelewa na kupewa heshima za kiitifaki.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

Trending Articles