Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal amesema Tanzania inatamani kuona hali ya utulivu na amani inarejea Syria na nchi kuendelea kujenga uchumi.
Kauli hiyo aliitoa jana wakati alipokutana na Balozi wa Syria nchini, Abdulmonem Annan, Ikulu jijini Dar es Salaam. Bilal pia alikutana na Balozi wa Oman, Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish
Bilal alisema kuwa msimamo wa Tanzania, unabakia katika kutaka pande zinazohusika katika mgogoro huo, zinafikia suluhu kwa amani ili wananchi wengi wasipoteze maisha.
Aidha, Balozi wa Syria, Annan alisema nchi yake iko katika kipindi kigumu na kwamba kwa sasa inatafuta kila linalowezekana kurejesha amani.
“ Kwa sasa tunahitaji msaada wa kimataifa kusaidia kuweka pande zote zinazokinzana mezani, kwa lengo la kufikia maazimio yatakayoifanya nchi hiyo isiparanganyike.”
Katika hatua nyingine, Balozi wa Oman, Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish alisema uhusiano kati ya Tanzania na Oman, unazidi kuimarika na kwamba wawekezaji kutoka Oman wamekuwa wakija kwa wingi.
“Ikiwa ni tofauti na siku za nyuma, kwa sasa wawekezaji wengi wanatoka Oman na kuja kuwekeza na Tanzania imeonesha kufungua milango kwa uwekezaji mkubwa na wa kati,” alisema.