Mji Mkongwe wa Zanzibar unadaiwa kuwa katika hatari ya kuondolewa kwenye ramani ya Hifadhi ya Urithi wa Kimataifa.
Hali hiyo inatokana na hujuma zinazofanywa na watu wasiofahamika kwenye miundombinu yake, ikiwemo nguzo za taa.
Hadhari hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe Zanzibar, Issa Sarboko Makarani.
Alisema vitendo hivyo havipaswi kufumbiwa, kwa kuwa vinahatarisha hadhi ya mji huo.
Miongoni mwa vitendo vinavyoharatisha mji huo kuondolewa kwenye orodha ya urithi, ni uharibifu wa nguzo za taa ambazo kwa mujibu wake zimevunjwa na kung’olewa kwa makusudi kwa ajili ya kupata chuma chakavu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Makarani alionesha waandishi wa habari baadhi ya maeneo ambayo nguzo za taa na zilizowekwa kuingia ndani ya vichochoro vya mji huo, zimeng’olewa.
Alisema vitendo vya aina hiyo, haviwezi kuachwa na kuvumiliwa, kwa sababu vinaharatisha hadhi ya mji huo ulio chini ya Hifadhi ya Urithi wa Kimataifa.
“Uongozi wa Mamlaka ya Mji Mkongwe umesikitishwa sana na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu kuvunja nguzo za taa pamoja na miundo mbinu mengine na kuitumia kwa matumizi ya vyuma chakavu,” alisema.
Wakati huo huo, Makarani alisema wanatarajia kufanya ukaguzi wa ndani katika Hoteli ya African House iliyopo katika eneo la Mji Mkongwe ili kuona kama kuna uharibifu wa usanifu wa jengo hilo sehemu za ndani.
Alisema kwa mujibu wa sheria za Mji Mkongwe, ruhusa ya kufanya ukarabati na usanifu wa majengo yaliyomo katika uhifadhi wa mji, inatakiwa kutolewa na taasisi yake.
“Hayo ndiyo maagizo ya Shirika la Umoja wa Kimataifa la (UNESCO) ambalo linasimamia usanifu wa majengo yaliyomo katika urithi wa Kimataifa,” alisema.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar, Abeid Juma alikiri kuwepo kwa vitendo vya hujuma, vinavyofanywa na baadhi ya watu katika eneo la Hifadhi ya Mji Mkongwe Zanzibar.
Alitaja pia wizi wa mifuniko ya makaro kuwa ni miongoni mwa matatizo makubwa, kutokana na wahusika kuitumia kwenye chuma chakavu.
Mji Mkongwe wa Zanzibar uliingizwa katika orodha ya miji yenye hadhi ya urithi wa kimataifa duniani mwaka 2000, huku vigezo muhimu ni kuwepo kwa soko kuu la watumwa la Mkunazini na makanisa ya kale na uhifadhi wake uliodumu hadi sasa.