Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) imefungua milango ya kujisajili kwa watahiniwa wa kujitegemea, wanaopenda kufanya mtihani wa Kidato cha Sita Mei mwakani.
Ofisa Habari wa Necta, John Nchimbi alisema usajili huo ni wa miezi mitatu kuanzia Julai Mosi hadi Septemba 30, mwaka huu.
Alisema ada ya kujisajili imepangwa kuwa Sh 50,000 na baada ya hapo, watahiniwa watasajiliwa kwa ada ya Sh 65,000, ikiwa ni ada na faini ya kuchelewa.
“Waombaji wote wanatakiwa kuzingatia hili kwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz.” alisema.
Nchimbi alisema kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mtihani, kuchukua namba rejea zinazotolewa bure na kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au M-Pesa.