Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

MALKIA WA SWAZILAND AIPA SEKONDARI SHILINGI MILIONI 5

$
0
0
Mke wa  Mfalme wa Swaziland, Malkia Nomsa Matsebula ameipatia Shule ya Sekondari ya Wama-Nakayama iliyopo Kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani,  zaidi ya Sh milioni tano kusaidia wanafunzi wa shule hiyo katika mahitaji yao ya kila siku.
Malkia Matsebula ambaye ni mke wa Mfalme Muswati  alitoa fedha hizo jana wakati alipotembelea shule hiyo ya bweni  inayopokea yatima na wanaotoka  kwenye familia maskini kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
Akizungumza  na wanafunzi hao, Matsebula alitaka wanafunzi hao kutumia nafasi hiyo kusoma kwa bidii.  Aliwaasa kusoma masomo ya aina mbalimbali ili hapo baadaye waweze kuwa   na taaluma mbalimbali.
 Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete alimshukuru Matsebula kwa kutembelea shule hiyo na kusema kuwa tafiti zinaonesha kuwa kama mtoto wa kike atapata  elimu ya kutosha tatizo la ndoa za utotoni, vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano vitapungua.
Mama Kikwete ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), inayoendesha shule hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles