Aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya nchini, Ismail Nwairat, amekufa, baada ya kujipiga risasi.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam, imeeleza kuwa balozi huyo alijiua ofisini kwake kwa kujipiga risasi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Wizara ilipokea taarifa kutoka ubalozi huo wa Libya ambayo ilifafanua kuwa Balozi Nwairat alijiua juzi saa saba mchana ofisini kwake katika jengo la Ubalozi wa Libya mtaa wa Mtitu, Upanga jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa Balozi Nwairat alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto.
“Maofisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlipuko wa bunduki na kumkuta Balozi Nwairat ameanguka chini, walimkimbiza hospitali ya AMI Oysterbay, ambako alitangazwa kuwa alikufa na Polisi walithibitisha kifo hicho,” ilieleza taarifa hiyo.
Kwa sasa mwili wa kiongozi huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na hadi sasa haijafahamika sababu ya balozi huyo kujiua.
Ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu Nwairat kwenda nyumbani kwao Libya kwa maziko Serikali imeuhakikishia Ubalozi wa Libya Ushirikiano wake katika kipindi chote kigumu cha msiba huo.