Mkazi wa Kijiji cha Mwamkulu wilayani Mpanda, Suzana Kingi (40), ameuawa kikatili na watu wasiofahamika kwa kuchinjwa akiwa katika chumba alicholala, huku mkwe wake akishuhudia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alisema jana kuwa mauaji hao ya kinyama, yanahusisha imani za kishirikina na yalitokea juzi usiku wa manane nyumbani kwa marehemu katika Kijiji cha Mwamkulu.
Kidavashari alisema usiku huo wa tukio, Suzana alikuwa amelala peke yake nyumbani kwake, jirani na nyumba walimolala wake wa mwanawe, Paul Charles, ambao ni Maria Kanyungiro na Maria Nsabi.
Ilidaiwa kuwa wakati mke wa kwanza, Maria Kayungiro akiwa chumbani kwake, alisikia mama mkwe akikimbia kutoka nyumbani kwake akienda kwenye nyumba walimokuwa wamelala wakweze, huku akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema ‘mama nakufa ....nakufa... nisaidieni.’
Mama mkwe wake alipofika katika nyumba walimolala wakweze, alisukuma kwa nguvu mlango wa chumba alichokuwa amelala mke wa pili, Maria Nsabi na kuingia chumbani huku akihema kwa hofu na akiendelea kupiga mayowe.
Kamanda Kidavashari alidai kuwa watu hao, ambao hawakufahamika mara moja wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mapanga, walikuwa wakimfuata kwa nyuma wakimfukuza.
Inadaiwa wauaji waliingia ndani ya chumba hicho, wakitumia mwanga wa kurunzi na kumkuta Suzana amejilaza na mke huyo wa pili wa mwanawe kitandani.
Kwa mujibu wa madai ya Kamanda Kidavashari, wauaji hao walianza kumshambulia Suzana kwa mapanga na hatimaye kumchinja.
Mke wa pili wa mwanawe, Nsabi, alishuhudia unyama huo kimya kimya, kwa madai kuwa alionywa asipige kelele na kwamba kama angejaribu, angeuawa kama mama mkwe wake, Suzana.
“Ilipotimu saa kumi alfajiri, Paul alirejea nyumbani kwake akitokea harusini katika kijiji cha jirani na alipoingia chumbani kwake, alimkuta mkewe Maria Nsabi akiwa amezirai sakafuni.
“Akiwa hajajua cha kufanya akajikuta amekaa kitandani ghafla akamwona mama yake mzazi akiwa ametapakaa damu mwili mzima tayari ameaga dunia,“ alieleza Kamanda Kidavashari.
Uchunguzi wa awali wa mkasa huo, kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, unaonesha kuwa chanzo za mauaji hayo ni imani za kishirikina na mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusishwa na tukio hilo.
Kidavashari amewaasa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuweza kuwabaini wahalifu hao ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.