Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

VETA SASA YAGEUKIA AJIRA SEKTA YA GESI

$
0
0
Mamlaka ya Elimu Tanzania (VETA) imesema imeanza kuboresha baadhi ya mitaala yake ili kuwezesha wanafunzi wake kupata ajira katika sekta za gesi na mafuta zilizogundulika hivi karibuni nchini.Mtaalamu wa Tathmini ya Mafunzo wa chuo hicho, Joyce Mwinuka alisema hayo katika maonesho ya kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.Alisema wakati wakiendelea kupanua wigo kwa kuongeza ufundishaji wa masafa marefu kwa wasiofikika, pia wanaangalia mitaala yao na kuiboresha iendane na mazingira yaliyopo kwa ajili ya kusaidia kupata ajira.Alisema ugunduzi wa mafuta na gesi nchini ni sekta mpya, hivyo wameanza kuboresha mitaala kukamata soko hilo la ajira na kutowaachia watu kutoka nje ya nchi.Alisema katika kupanua wigo wameanza kutoa mafunzo kwa wanafunzi kuingia asubuhi na wengine kuingia mchana ili kuongeza udahili na kujenga vyuo katika mikoa yote.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles