Jeshi la Magereza limepata leseni 102 za uchimbaji wa madini ya ujenzi katika maeneo mbalimbali ya magereza nchini.
Madini ambayo jeshi hilo litafanya uchimbaji ni pamoja na chokaa, mawe, kokoto, mchanga na moramu.
Leseni hizo zitatumika kuingia ubia na wawekezaji wenye nia ya dhati ya kushirikiana na jeshi hilo katika madini hayo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja alisema hayo jana kwenye hafla ya kuaga wastaafu wa jeshi hilo jijini hapa.
Alitaka wastaafu hao kuwa mabalozi wa magereza ikiwa ni pamoja na kufuatilia kwa karibu maendeleo yake na utendaji wake wa kazi.
Minja alisema upatikanaji wa leseni ni mojawapo ya hatua ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili, hususani katika kuipunguzia Serikali gharama za kuhudumia magereza.
Alisema vyanzo vilivyobuniwa kuongeza tija ni pamoja na kuingia ubia na wawekezaji wenye nia nzuri na jeshi.
“Katika kuhakikisha kuwa tunaimarisha na kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo, Jeshi la Magereza limeingia ubia na baadhi ya kampuni za ndani na nje ya nchi ili kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji,” alisema.
Wakati huo huo alitoa mwito kwa wastaafu kuwa mabalozi wazuri wa jeshi hilo. “Nawasihi wastaafu muendelee kuwa mabalozi wazuri wa Chombo hiki hasa kwa kipindi ambapo Jeshi hili liko katika harakati za maboresho ya kuwezesha kuliendesha kisayansi na kiweledi na hatimaye kufikia malengo yanayotarajiwa,” alisema.