Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

BREAKING NEWS!!! MAJAMBAZI WASHAMBULIA KWA RISASI BASI LA MAHABUSU

$
0
0
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba watu wenye silaha wanaoaminika kuwa ni majambazi wamelishambulia kwa risasi basi lililokuwa limebeba mahabusu maeneo ya Mikocheni, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, majambazi hayo yanayoaminika kuwa yalijibanza kusubiria basi hilo, yaliibuka ghafla na kuanza kumimina risasi kuelekea kwenye basi hilo hali iliyomlazimisha dereva wa basi hilo kusimamisha basi hilo kunusuru maisha yake.
Huku majambazi hayo yakiendelea kumimina risasi, mahabusu waliokuwamo kwenye basi hilo walifanikiwa kutoroka na kutokomea kusikojulikana.
Haikuweza kufahamika mara moja idadi ya mahabusu hao waliotoroka wala majeruhi wowote waliotokana na shambulizi hilo la aina yake.
Habari zaidi zitawajia hapa hapa muda mfupi ujao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles