Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti jijini Dar es salaam.
Katika tukio la kwanza lililotokea Juni 30 saa 12 asubuhi huko barabara ya Bagamoyo eneo la Tegeta gari isiyofahamika ilimgonga mwanaume mmoja asiyefahamika anaekadiriwa kuwa na miaka (30-35).
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi Kinondoni Camillius Wambura alisema gari hilo lilikuwa likitokea Tegeta Kibaoni lilimgonga mwanaume huyo na alikufa papo hapo alivaa suruali ya rangi ya ugoro na fulana nyekundu, mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala dereva anatafuta baada ya kutoweka eneo la tukio.
Katika tukio la pili moto ulizuka gafla na kuteketeza duka la nguo Kariakoo mtaa wa Mchikichini /Kongo.
Tukio hilo lilitokea saa 11 ambapo moto uliteketeza duka mali ya Seif Suleiman (32) mkazi wa Sinza Vatican.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi Ilala Marietha Minangi alisema moto uliteketeza mali zote ambazo thamani yake haijafahamika, pia uliunguza pesa taslimu Sh milioni 1.5 moto ulizimwa na zimamoto na kikosi cha uokoaji cha jiji kwa kusaidiana na wananchi, hakuna madhara kwa binadamu.