Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

WIZI WA NYAYA WASITISHA MAWASILIANO IKULU

$
0
0
Wizi wa nyaya za Kampuni ya Simu nchini (TTCL) na zile zinazounganishwa kwenye transfoma za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) umesababisha ukosefu wa huduma ya mawasiliano ya uhakika ikiwamo Ikulu ndogo ya Lubaga mkoani hapa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Meneja wa Shirika la Simu mkoani Shinyanga, Peter Kuguru alisema wizi wa nyaya za simu za mkonga wa chini ulianza tangu mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu, katika maeneo ya Ngokolo kwa kuibiwa nyaya 1,000, hali iliyosababisha eneo la Ikulu ndogo lililoko Lubaga kukosa mawasiliano ya simu.
Naye Meneja wa Tanesco wa Mkoa wa Shinyanga, Maugira Mgamba alisema wizi huo wa nyaya, umesababisha shirika lake  kuingia hasara kiasi cha Sh milioni 8.
Meneja huyo alisema kuwa hujuma na wizi huo umekuwa ukikithiri na kusababisha huduma za mawasiliano ya simu za mezani kukosekana na kusababisha hasara kwa wenye viwanda hasa vile vinavyochambua pamba na kutengeneza maji.
Akivitaja  viwanda hivyo kuwa ni  Kisumo Ginnery Ltd., Ahamu Ginnery Ltd, Fresh Investment Ltd, Jambo Group Ltd, GAKI Investment Limited, Afrisian Ginnery Ltd na viwanda vya nguo na ngozi vinavyojengwa na Wachina katika eneo hilo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

Trending Articles