Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

SAMAKI WA 'KICHINA' WAPIGWA MARUFUKU ZANZIBAR

$
0
0
Bodi ya Chakula Madawa na Vipodozi imepiga marufuku uuzwaji  katika maeneo ya wazi kwa samaki walioingizwa nchini kutoka China na Kampuni ya Kauthar Sea food Ltd mjini Unguja kwa sababu za kiafya.
Mrajisi wa Bodi ya Madawa na Vipodozi, Burhani Simai alisema kwa kulinda afya za watumiaji, samaki hao hawaruhusiwi kuuzwa sehemu za wazi ikiwemo katika masoko, magari yanayotembea pamoja na ndani ya wachuuzi.
Akifahamisha zaidi, Simai alisema samaki hao wanatakiwa kuuza katika sehemu za hifadhi yake ikiwemo mitambo ya baridi kwa ajili ya uhifadhi.
“Bodi ya Madawa na Vipodozi inawataka watu wanaouza samaki hao kuhakikisha kwamba wanakuwa katika hifadhi yake ya kudumu yenye mitambo baridi tofauti na sasa kuuzwa kwa kutembezwa barabarani na katika magari,” alisema.
Hata hivyo, Simai alisema kwamba samaki hao wapo salama na wameingizwa wakiwa katika viwango vinavyokubalika baada ya kufanyiwa utafiti.
Kwa mfano, alisema samaki hao walichunguzwa na Mamlaka ya Chakula nchini na Tanzania Atomic Energy Commision iliopo Arusha na kupewa kibali na Shirika la Uvuvi la Tanzania.
Alisema walipoingizwa nchini, walipewa kibali na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Bodi ya Chakula na Vipodozi lakini kwa kufuata masharti maalumu.
Hata hivyo, alisema kwa bahati mbaya samaki hao wanauzwa mitaani kiholela kinyume na maelekezo yaliyokubaliwa awali.
“Tunawaomba wahusika wa samaki hao kuhakikisha kwamba wanafuata masharti yaliyofikiwa awali yanayotokana na kibali chake,” alisema Simai.
Samaki wa 'kichina'wamekuwa wakinunuliwa na watu mbalimbali huku wakisaidia tatizo la uhaba wa samaki linalotokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ya upepo mkali unaovuma hivi sasa.
“Hawa samaki wanatusaidia sana kukabiliana na tatizo la uhaba wa samaki kwa sasa hata bei yake sio kubwa,” alisema mnunuzi mmoja katika soko la Darajani ambapo samaki mmoja anauzwa kati ya Sh 1,000 hadi 1,500.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

Trending Articles