Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

ALAT YAKUSANYA BILIONI 1.5/- KUMALIZA UHABA WA MADAWATI

$
0
0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa nchini (ALAT), Dk Didas Massaburi amesema wamekamilisha awamu ya kwanza ya mpango wao wa kukusanya Sh bilioni 1.5 kwa ajili ya kumaliza tatizo la uhaba wa madawati unaozikabili shule za msingi nchini.
Pia ALAT inafikiria kutengeneza madawati kwa kutumia plastiki ngumu badala ya mbao ili kukomesha vitendo vya ubadhirifu unaofanywa na baadhi ya wahusika wanaoratibu miradi ya madawati kwenye halmashauri nchini na kusababisha madawati mengi kuharibika muda mfupi baada ya kukabidhiwa shuleni.
Ametoa kauli hiyo jijini Tanga jana alipowasilisha taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mwenendo wa Maonesho ya Kitaifa ya 30 ya shughuli za halmashauri katika kusherehekea Siku ya Serikali za Mitaa nchini inayohitimishwa leo ambapo mwaka huu inasherehekewa jijini Tanga katika Uwanja wa Tangamano.
Alisema kuanza kwa mchakato wa kukusanywa kwa fedha hizo ni matokeo ya awali ya hatua zinazochukuliwa na ALAT kutekeleza agizo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alilolitoa wakati alipofungua mkutano mkuu wa mwaka huu wa jumuiya hiyo.
Waziri Mkuu aliitaka ALAT kubuni na kutekeleza mipango endelevu itakayomaliza kwa haraka tatizo lililopo sasa la uhaba wa madawati milioni 1.5 kwenye shule mbalimbali za msingi nchini.
Massaburi alisema takwimu zinaonesha kwamba tatizo la madawati ni changamoto kubwa ambalo halijapatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu kwenye halmashauri zote nchini na limesababisha wanafunzi wengi kuendelea kuketi sakafuni na kwenye vumbi huku halmashauri zikishindwa kuwa na mikakati ya kuliondoa tatizo hilo.
Hata hivyo, Massaburi alisema ALAT inafikiria kutengeneza madawati hayo kwa kutumia plastiki ngumu ili kukabiliana na changamoto ya ubadhirifu wa fedha unaosababishwa na usimamizi mbovu kwenye halmashauri wakati wa utekelezaji wa miradi ya kutengeneza madawati kwa kutumia mbao ambazo ziko chini ya kiwango cha ubora unaotakiwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles