![]() |
Kazi ya uchimbaji madini ikiendelea huko Geita. |
Hatua hiyo imetokana na kasoro mbalimbali zilizopo katika mikataba hiyo, hususan katika maeneo ambayo sheria haifuatwi, ikiwemo tozo katika Halmashauri.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Maselle alisema hayo jana alipokuwa akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 40 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, yaliyofanyika katika chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Alisema kwa muda mrefu, kumekuwa na malalamiko ya sekta hiyo, kutonufaisha nchi, jambo lililofanya serikali kufanya mazungumzo na wawekezaji wakubwa ili kuweza kufuata sheria.
Alisema baadhi ya masuala ambayo yamekuwa na utata ni pamoja na tozo ya ushuru, ambayo kampunihizo hulipa Sh 200,000 badala ya asilimia 0.3 ya mapato yao.
Maselle alisema mazungumzo ya kurejea mikataba hiyo, yamekamilika hasa katika tozo na kodi na maeneo mengine na wiki ijayo watatangaza rasmi kuanza kurejea mikataba hiyo.
“Katika kurejea mikataba hiyo ambayo ilishafungwa tutaangalia hasa masuala ya kodi na tozo ili kuweza kutozwa kwa mujibu wa sheria,” alisema.
Aidha, Maselle alitoa wito kwa menejimenti ya chuo hicho, kutayarisha mikakati na kuonana nakampuni za gesi na mafuta ili kuweza kuandaa mitaala inayoendana na mahitaji yao.
Alitaka kuangalia zaidi katika kushughulikia masuala ya mahusiano ya kijamii na masuala ambayo yatakuwa hitaji katika sekta hizo za mafuta na gesi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Jakaya Kikwete alitoa wito kwa Taasisi hiyo kuhakikisha haki na ustawi wa Tanzania na hasa kwa makundi maalumu zinadumishwa na kuendelezwa.
Rais Kikwete alisema hayo katika Hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, ambapo aliwataka kutoa Mafunzo yanayolenga katika kugusa nyanja mbalimbali za maisha na jamii yetu.
“Ni ukweli usiopingika kwamba, mafunzo yanayotolewa na Taasisi ya Ustawi wa Jamii yana mchango mkubwa katika maendeleo ya Ustawi wa Jamii yetu kwa ujumla, hii nikutokana na kuongezeka kwa matatizo katika jamii yetu ambayo utatuzi wake unategemea sana programu zinazotolewa katika taasisi hii,” alisema.
Kikwete alisema baadhi ya matatizo hayo ni ongezeko kwa watoto wa mitaani, ongezeko la kupungua kwa maadili sehemu ya kazi, kuvunjika kwa ndoa, kuongezeka kwa watu wanaoishi kwa kipato cha chini na changamoto zinazotokana na ugojwa wa Ukimwi.
“Yote haya utatuzi wake kwa kiasi kikubwa unategemea sana wataalamu wanaohitimu katika taasisi hii, vile vile ninatambua kwamba ili kufikia malengo ya milenia, Diraya Taifa 2025 na programu nyingine za kijamii, Kitaifa na Kimataifa, Taasisi hii inayo nafasi kubwa katika kufanikisha kufikia malengo ya programu hizi,” alisema.
Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Chuo hicho, Profesa Lucian Msambichaka alisema Oktoba mwakaHuu, wataanzisha Shahada ya Uzamili katika fani ya Ustawi wa Jamii baada ya kupata ithibati ya NACTE kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Alisema pia mwezi ujao, wanatarajia kuanza kutumia jengo la Maabara lililozinduliwa jana, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo pamoja na kuendeleza eneo la chuo hicho lenye ukubwa wa ekari 500 lililopo Msoga wilaya ya Bagamoyo, ikiwa ni kampasi ya pili ya taasisi hiyo.